Apr 21, 2024 08:04 UTC
  • Abdul Malik al Houthi: Saudia imeondoa aya za Qur'ani katika vitabu vya kiada ili kuwaridhisha Wazayuni

Mkuu wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen amewatuhumu viongozi wa Saudi Arabia kuwa wameondoa baadhi ya mafundisho ya Qur'ani katika progamu za kufundishia mashuleni ili kuwaridhisha Wazayuni.

Abdul Malik al Houthi amesema kuwa utawala wa Saudi Arabia umeondoa aya za Qur'ani katika vitabu vya mtaala mashuleni (Syllabus) ili kuepuka kuwakasirisha Wazayuni. Amesema, aya hizo zinazochujwa na Saudia mashuleni ni zile zinazozungumzia jinai zilizotendwa na Wayahudi.  

Qur'ani Tukufu 

Afisa huyo wa Yemen ameongeza kuwa utawala wa Saudi Arabia hata umeondoa kikamilifu au baadhi ya sejemu za  suna za Mtume  Muhammad (s.a.w) katika programu za kielimu mashuleni na kusema kuwa hatua hiyo ya Saudia ni dhulma kwa vizazi vijavyo. 

Al Houthi ameongeza kuwa Saudia imefanya hivi sambamba na mpango wake wa kuhuisha  uhusiano na utawala wa Kizayuni. 

Umoja wa Falme za Kiarabu pia umefuata mkondo huu wa Saudia ambapo vitabu vya kufundishia katika shule nchini humo huzungumza kwa maslahi ya Wazayuni katika jitihada za Imarati za kulea kizazi ambacho ni rafiki kwa Israel. 

 

Tags