Nov 05, 2020 03:57 UTC
  • Bunge la Iraq kuanza kujadili mauaji ya kigaidi ya Luteni Qasem Soleimani

Mjumbe mmoja wa Kamisheni ya Usalama na Ulinzi ya Bunge la Iraq amesema kuwa, karibuni hivi bunge hilo litaanza kujadili faili la kuuliwa kigaidi na Marekani, Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Abu Mahdi al Muhandis na mashahidi wenzao wanane.

Badr al Ziyadi alisema hayo jana (Jumatano) alipohojiwa na mtandao wa habari wa al Maaluma na kuongeza kuwa, uchunguzi maalumu kuhusu jinai iliyofanywa na Marekani, ya kumuua shahidi Hajj Qassem Soleimani, Kamand wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (SEPAH) na shahid Abu Mahdi al Muhandis, Naibu wa Mkuu wa harakati ya wananchi ya al Hashd al Shaabi na mashahidi wenzao wanane, utaanza kufanywa na Bunge la Iraq wiki ijayo.

Luteni Jenerali Qassem Soleimani ambaye tarehe 3 Januari mwaka huu alikwenda nchini Iraq akiwa mgeni rasmi wa serikali ya nchi hiyo, aliuliwa kidhulma na kikatili na wanajeshi magaidi wa Marekani, karibu na uwanja wa ndege wa Baghdad akiwa pamoja na Abu Mahdi al Muhandis na wanamapambano wengine wanane.

Bunge la Iraq lilipopasisha kutimuliwa wanajeshi magaidi wa Marekani nchini humo

 

Faili hilo linahusiana na uhalifu wa Marekani wa kufanya mauaji hayo ya kigaidi katika nchi nyingine, dhidi ya mgeni rasmi wa nchi hiyo. Kabla ya hapo Bunge la Iraq lilishapasisha muswada wa kutimuliwa wanajeshi wote wa Marekani nchini humo.

Uongozi wa Bunge la Iraq umewataka wabunge waainishe muda wa kukutana na Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Mustafa al Kadhimi, ili kujadiliana naye masuala mbalimbali ikiwemo kuuliwa shahidi Luteni Jenerali Soleimani na Abu Mahdi al Muhandis pamoja na ratiba ya kuondoka wanajeshi wa Marekani nchini Iraq.

Tags