Apr 02, 2016 04:40 UTC
  • Saudi Arabia yaendelea kutenda jinai dhidi ya wananchi wa Yemen

ndege za kijeshi za Saudi Arabia cimeendelea kufanya mashambulio katika maeneo mbalimbali ya Yemen.

Habari kutoka nchini Yemen zinasema kuwa, miji mbalimbali ya nchi hiyo imeendelea kuandamwa na mashambulio ya anga ya Saudia na washirika wake na kusababisha mauaji na uharibifu mkubwa. Aidha ripoti kutoka Yemen zinasema kuwa, hali ya kibinadamu katika nchi hiyo inazidi kuwa mbaya siku baada ya siku.Hivi karibuni Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Human Rights Watch na asasi nyingine saba zilitoa ripoti ya pamoja ambayo mbali na kuashiria jinai za kivita huko Yemen ilitaka Saudia iwekewe vikwazo vya silaha.

Saudi Arabia kwa kushirikiana na nchi kadhaa, ilianzisha mashambulizi ya kivamizi mwezi Machi mwaka jana kwa lengo la kuwashinikiza raia wa Yemen kumkubali kibaraka wake Abd Rabbuh Mansur Hadi, aliyekuwa rais wa nchi hiyo na aliyetangaza kujiuzulu na kukimbilia Saudia. Hata hivyo hujuma hizo hazijafanikiwa kutokana na Wayemen kuendelea kusimama imara dhidi ya njama hizo chafu za Saudia.

Tags