Hamas: Mapinduzi ya Kiislamu yameipa nguvu Intifadha ya Palestina
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i1009-hamas_mapinduzi_ya_kiislamu_yameipa_nguvu_intifadha_ya_palestina
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas imesema Mapinduzi ya Kiislamu yaliyotokea mwaka 1979 nchini Iran yameishajiisha na kuipa nguvu Intifadha na mapambano ya Wapalestina dhidi ya utawala wa kizayuni wa Israel ambao unazikalia ardhi za Wapalestina kwa mabavu.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Feb 11, 2016 07:21 UTC
  • Hamas: Mapinduzi ya Kiislamu yameipa nguvu Intifadha ya Palestina

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas imesema Mapinduzi ya Kiislamu yaliyotokea mwaka 1979 nchini Iran yameishajiisha na kuipa nguvu Intifadha na mapambano ya Wapalestina dhidi ya utawala wa kizayuni wa Israel ambao unazikalia ardhi za Wapalestina kwa mabavu.

Khalid Qadoumi, mwakilishi wa Hamas hapa nchini amesema harakati za Wapalestina za kupinga dhulma na kupokonywa ardhi yao zimeshajiishwa na Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran. Qadoumi amepongeza Iran kwa kuendelea kusimama pamoja na Wapalestina huku akiutaja uhisiano kati ya pande mbili hizo kuwa dhabiti na wa kimaanawi. Mwakilishi wa harakati ya Hamas hapa nchini ameashiria zama ambapo Misri ilifikia mwafaka na utawala haramu wa Israel na kusisitiza kwamba, Iran ya Kiislamu ilisimama na Wapalestina na kuungana mkono mwamko na harakati zao dhidi ya wazayuni maghasibu.

Hii leo Iran inaadhimisha miaka 37 ya Mapinduzi ya Kiislamu, ambapo wananchi chini ya uongozi wa Ayatullah Ruhullah Khomeini walihitimisha kipindi cha giza totoro katika historia ya Iran kwa kuung'oa madarakani utawala wa kidikteta wa Shah Pahlavi.