Sababu za siri za umwagaji damu wa Israeli huko Gaza
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i105006-sababu_za_siri_za_umwagaji_damu_wa_israeli_huko_gaza
Mauaji ya halaiki na ya kizazi yanayofanywa na utawala wa kigaidi wa Israel huko Gaza yameingia katika siku yake ya arubaini na tano, huku taasisi za kieneo na kimataifa zikiwa zimekaa kimya na hivyo kuupa utawala huo alama ya taa ya kijani kwa ajili ya kuendeleza jinai zake hizo dhidi ya raia wasio na hatia.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 20, 2023 03:50 UTC
  • Sababu za siri za umwagaji damu wa Israeli huko Gaza

Mauaji ya halaiki na ya kizazi yanayofanywa na utawala wa kigaidi wa Israel huko Gaza yameingia katika siku yake ya arubaini na tano, huku taasisi za kieneo na kimataifa zikiwa zimekaa kimya na hivyo kuupa utawala huo alama ya taa ya kijani kwa ajili ya kuendeleza jinai zake hizo dhidi ya raia wasio na hatia.

Tangu kuanza hujuma ya pande zote ya jeshi la Kizayuni dhidi ya Gaza mnamo tarehe 7 Oktoba, zaidi ya Wapalestina 12,000 wameuawa kwa umati wengine wao wakizikwa wakiwa hai katika ardhi hiyo ndogo lakini yenye watu wengi zaidi duniani, ambapo zaidi ya 5000 kati yao ni watoto na zaidi ya 3,500 ni wanawake.

Zaidi ya Wapalestina 30,000 wamejeruhiwa, ambapo wengi wao wamenyimwa fursa ya kupata huduma hospitalini na sasa wanakabiliwa na hatari ya kifo kwa sababu hospitali 21 kati ya 36 za Gaza zimeharibiwa kabisa kwa kulipuliwa na jeshi la utawala wa Kizayuni. Maelfu kadhaa ya watu waliojeruhiwa na kupelekwa katika hospitali ya Shifa baada ya kukamatwa na jeshi la Israel, wamehamishiwa sehemu isiyojulikana na kuna uwezekano hawatapatikana kabisa.

Wanawake wajawazito elfu 52 wako katika hali mbaya na hawataweza kujifungua katika mazingira salama. Watoto elfu 30 wanaozaliwa na mama zao wanaonyonyesha hawapati maji salama wala safi ya kutumia.

Zaidi ya watu 2,700 wangali bado wako chini ya vifusi, ambapo takriban 1,350 kati yao ni watoto.

Kufuatia mashambulizi ya jeshi la Kizayuni, zaidi ya nyumba elfu 41 za makazi huko Gaza zimeharibiwa kabisa na nyingine zaidi ya laki mbili ziko katika hali mbaya isiyo salama kuishi wanadamu.

Mauaji na uharibifu wa makusudi wa Wazayuni katika Ukanda wa Gaza

Takriban watu milioni 1 moja na laki saba kati ya jumla ya wakazi milioni mbili na laki nne wa Gaza, ambao wanaunda takriban asilimia 80 ya wakazi wa eneo hilo, sasa wameyahama makazi yao, na mamia ya maelfu yao wamehamia kwenye kambi za wakimbizi za Umoja wa Mataifa kusini mwa Gaza ambapo wanaishi katika mazingira ya kuhuzunisha mno.

Maafa makubwa yanayosababishwa na mashambulizi ya kinyama ya utawala wa Kizayuni dhidi ya watu wa Gaza hayawiani kabisa na operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa, ambapo nyaraka mpya zilizofichuliwa karibuni zinaonyesha kuwa baraza la mawaziri lenye itikadi kali la Netanyahu tayari lilikuwa limetayarisha mpango wa kuanzisha mashambulio makubwa dhidi ya Gaza kabla hata ya kufanyika operesheni hiyo na kwamba lilikuwa linatafuta tu kisingizio cha kutekeleza mpango huo.

Moja ya nyaraka hizo zilizochapishwa na gazeti la Haaretz zinaonyesha kuwa shambulio dhidi ya tamasha la muziki katika mji wa "Raim" mnamo Oktoba 7 halikutekelezwa na Hamas bali lilifanywa na helikopta ya utawala wa Israeli, ambapo lilisababisha vifo vya watu 364.

Kwa mujibu wa Haaretz, uchunguzi unathibitisha kwamba vikosi vya Hamas havikuwa na habari kuhusu tamasha hilo la muziki tarehe 7 Oktoba, bali ni helikopta ya Apache ya Israel ndiyo ililenga washiriki wa tamasha hilo karibu na Ukanda wa Gaza.

Kwa mujibu wa ushahidi mwingine, lengo la mwisho la Wazayuni sio tu kuwafukuza Wapalestina katika ardhi yao, bali pia ni kunyakua akiba ya nishati ya gesi yenye thamani ya mabilioni ya dola huko Gaza, iliyogunduliwa mnamo 1999, pamoja na ile iliyoko katika eneo la Levant katika Bahari ya Mediterania ya Mashariki ambayo iligunduliwa mwaka 2013.

Pia, kwa mujibu wa waraka rasmi wa siri wa Wizara ya Intelijensia ya Israel ambao ulivuja Oktoba 13 ukiwa na nembo rasmi ya wizara hiyo, Wapalestina milioni 2 na laki mbili wanaoishi katika Ukanda wa Gaza wanapaswa kufukuzwa na kuhamishiwa katika Peninsula ya Sinai ya Misri, yaani kambi ya wakimbizi huko Misri, na hilo ni suala ambalo Israeli na Marekani tayari zimelipitisha.

Watoto, wahanga wakuu wa mauaji ya kizazi ya Wazayuni

Katika waraka huo wenye kurasa 10, kuna machaguo matatu ambayo yamependekezwa kuhusu mustakabali wa Wapalestina huko Gaza, ambapo chaguo linalopendelewa zaidi ni la kuhamishwa Wapalestina wote kutoka ukanda huo. Usahihi wa waraka huo umethibitishwa na Wizara ya Intelihensia ya Israeli.

Suala hilo linaonyesha wazi wazi kwamba, kinyume na madai na propaganda za watawala  na vyombo vya habari vya Kizayuni, mashambulio ya kikatili yanayoendelea hivi sasa huko Gaza hayana uhusiano wowote wala si jibu kwa operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa, bali yanafuatilia malengo ya kichokozi, uporaji na ya kujitanua utawala huo katika ardhi za Wapalestina, ambayo katika hatua ya kwanza, yanalenga kuondolewa Ukanda wa Gaza na kisha katika hatua ya pili kufutiliwa mbali kabisa Palestina katika ramani ya hivi sasa ya dunia.