Ban alaani mashambulizi ya kigaidi ya Baghdad
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amelaani mashambulizi ya kigaidi yaliyotokea Baghdad nchini Iraq na kutoa mkono wa pole na salamu za rambirambi kwa familia za wahanga wa mashambulizi hayo.
Taarifa iliyotolewa na Ban Ki-moon imesema mashambulizi hayo ni jinai ya kutisha. Taarifa hiyo pia imewataka Wairaqi kujiepusha na hatua yoyote inayoweza kuzusha hofu au kudhoofisha umoja wa kitaifa. Vilevile Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameitaka serikali ya Iraq kuwasaka na kuwatia nguvuni waliofanya mashambulizi hayo.
Ripoti zinasema kuwa mashambulizi mawili tofauti yaliyotokea jana katika wilaya ya Karrada mjini Baghdad yameua watu 176 na kujeruhi wengine karibu 200.
Kundi la kigaidi la Daesh limetangaza kuwa ndilo lililohusika na miripuko hiyo ya Baghdad.