Jun 16, 2024 07:37 UTC
  • Kiongozi wa upinzani wa Israel ataka kuuzuliwa Netanyahu

Kinara wa upinzani wa utawala wa Kizayuni wa Israel amesema wakati umefika wa kuiangusha serikali ya utawala huo inayoongozwa na Waziri Mkuu, Benjamin Netanyahu.

Yair Lapid amesema hayo na kuongeza kuwa, utawala wa Netanyahu unapasa kuangushwa kwa namna unavyoendeshwa ndivyo sivyo vita vya Gaza.

Lapid amesema wiki kadhaa zimepita, lakini Netanyahu na serikali yake wameshindwa kuwarejesha nyumbani kwa familia zao mateka wa Kizayuni walioko katika Ukanda wa Gaza.

Ametoa mwito kwa upinzani ndani ya utawala huo haramu kuungana kwa shabaha ya kulianguisha baraza la mawaziri la vita linaloongozwa na Netanyahu.

Hivi karibuni, Benny Gantz na Gadi Eisenkot, wajumbe wawili wa ngazi za juu wa baraza la mawaziri la vita la utawala wa Kizayuni walitangaza rasmi kujitoa kwenye baraza hilo. Aidha Hili Tropper ambaye ni mtu wa karibu na Gantz pia ametangaza rasmi kujitoa kwenye muungano unaounda serikali ya Netanyahu.

Yair Lapid

Haya yanajiri siku chache baada ya msemaji wa jeshi katili la utawala haramu wa Israel, Daniel Hagari kuiambia kanali ya 12 ya televisheni ya Kizayuni kwamba haliwezi kuwarejesha nyumbani mateka kupitia operesheni ya kijeshi.

Katika siku za hivi karibuni, walowezi wa Kizayuni wamekuwa wakiandamana kupinga na kulalamikia sera za Benjamin Netanyahu na kushindwa kwake kufikiwa mapatano ya kuachiwa huru mateka wa utawala wa kizayuni wanaoshikiliwa Ukanda wa Gaza. 

Tags