Ripoti: Mayatima wameongezeka Gaza baada ya Israel kuanzisha hujuma ya kijeshi
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i113312-ripoti_mayatima_wameongezeka_gaza_baada_ya_israel_kuanzisha_hujuma_ya_kijeshi
Ofisi ya vyombo vya habari ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina huko Gaza imetangaza ongezeko la maelfu ya watoto mayatima tangu kuanza kwa mashambulizi ya Wazayuni katika Ukanda wa Gaza Oktoba mwaka jana (2023).
(last modified 2024-06-24T22:59:09+00:00 )
Jun 24, 2024 22:59 UTC
  • Ripoti: Mayatima wameongezeka Gaza baada ya Israel kuanzisha hujuma ya kijeshi

Ofisi ya vyombo vya habari ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina huko Gaza imetangaza ongezeko la maelfu ya watoto mayatima tangu kuanza kwa mashambulizi ya Wazayuni katika Ukanda wa Gaza Oktoba mwaka jana (2023).

Karibu watoto 20,000 wa Kipalestina wamekuwa mayatima kufuatia jinai za kinyama za utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza.

Ripoti hiyo inaeleza kuuwa, zaidi ya 3% ya watoto hao ni mayatima wa baba na mama.

Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa wanawake wa Kipalestina zaidi ya elfu kumi wameuawa shahidi katika vita na mashambulizi ya jeshi la utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza.

Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa watoto 19,000 wa Kipalestina wamekuwa yatima kufuatia kuuliwa shahidi akina mama elfu sita katika mauaji ya kimbari ya Israel dhidi ya Gaza. 

Ripoti ya Umoja wa Mataifa imeongeza kuwa: Zaidi ya wanawake na wasichana milioni moja katika Ukanda wa Gaza hawana chakula na maji salama; na wanaishi katika hali mbaya sana ya kibinadamu. 

Wakati huo huo, Wizara ya Elimu ya Palestina imetangaza kuwa, moja ya matokeo ya vita dhidi ya ukanda wa Gaza kwa wanafunzi ni kukosa elimu wanafunzi 800,000 katika eneo hilo.

Katika upande mwingine, Francesca Albanese, Ripota wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Palestina, amesema katika taarifa kwamba hali ya maafa huko Ukanda wa Gaza imezidi kuwa mbaya. Kwa kauli yake, utawala haramu wa Israel unalenga misafara ya misaada ya kibinadamu inayotumwa Gaza na kuzuia ufikaji wa misaada katika ukanda huo.