Hamas: Facebook inahudumia malengo ya Wazayuni
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i11350-hamas_facebook_inahudumia_malengo_ya_wazayuni
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) imetangaza kuwa mtandao wa kijamii wa Facebook unafuata siasa na sera za kiadui za utawala wa Kizayuni wa Israel.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 16, 2016 02:16 UTC
  • Hamas: Facebook inahudumia malengo ya Wazayuni

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) imetangaza kuwa mtandao wa kijamii wa Facebook unafuata siasa na sera za kiadui za utawala wa Kizayuni wa Israel.

Msemaji wa HAMAS, Hosam Badran amesema hatua ya mtandao wa Facebook ya kufunga kurasa binafsi za viongozi wa harakati hiyo kwa mwaka wa sita sasa tangu kuanza kwa mapambano ya Intifadha dhidi ya maghasibu wa Isarel ni kufuata waziwazi siasa za kiadui za Wazayuni dhidi ya mapambano ya ukombozi ya wananchi wa Palestina.

Badran ameongeza kuwa, mtandao wa Facebook unatumia mbinu zote kukandamiza vyombo vya habari vya Palestina na kuzuia upashaji wa habari na ukweli wa mambo.

Msemaji wa harakati ya HAMAS amesema kuwa, adui Mzayuni ambaye ameshindwa kuzima mapambano ya Intifadha, anatumia mbinu zote kuzima sauti ya ukweli na haki na kukandamiza vyombo vya habari vya wapigania uhuru.