Ndege ya kivita ya Marekani yadunguliwa kwenye Bahari Nyekundu ikivamia Yemen
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i120468-ndege_ya_kivita_ya_marekani_yadunguliwa_kwenye_bahari_nyekundu_ikivamia_yemen
Kamandi Kuu ya Jeshi la Marekani (CENTCOM) imesema ndege yake ya kivita imedunguliwa kwenye Bahari Nyekundu katika kile ilichodai kuwa ni shambulizi la kimakosa kutoka jeshi lenyewe la Marekani, ikiwa katika operesheni yake dhidi ya Yemen kwa lengo la kuuunga mkono utawala wa Israel
(last modified 2024-12-22T09:19:03+00:00 )
Dec 22, 2024 09:19 UTC
  • Ndege ya kivita ya Marekani yadunguliwa kwenye Bahari Nyekundu ikivamia Yemen

Kamandi Kuu ya Jeshi la Marekani (CENTCOM) imesema ndege yake ya kivita imedunguliwa kwenye Bahari Nyekundu katika kile ilichodai kuwa ni shambulizi la kimakosa kutoka jeshi lenyewe la Marekani, ikiwa katika operesheni yake dhidi ya Yemen kwa lengo la kuuunga mkono utawala wa Israel

Taarifa hiyo imesema mapema Jumapili, ndege aina ya F/A-18F Super Hornet ilitunguliwa kimakosa, huku CENTCOM ikithibitisha katika taarifa yake kwamba marubani waliokuwa kwenye ndege hiyo wako salama.

Ndege hiyo iliyokuwa imeruka kutoka katika meli ya kivita inayosheheni ndege za kivita ya USS Harry S. Truman (CVN-75), ilikuwa ikiruka juu ya Bahari Nyekundu wakati ilipolengwa kwa kombora na kuanguka. Jeshi la Marekani limedia kuwa kombora hilo lilivurumishwa kutoka manoari yake  ya USS Gettysburg (CG-64). Hata hivyo madai hayo ya Marekani hayajathibitishwa kwa njia huru na yamkini ndege hiyo imeangushwa kwa makombora ya Jeshi la Yemen.

Katika miezi ya hivi karibuni jeshi la Yemen limefanikiwa kutungua ndege kadhaa za kivita zisizo na rubani za Marekani aina ya MQ9 ambayo kila inagharimu mamilioni ya dola.

Maeli za kivita za Marekani ziko katika  Bahari Nyekundu kulinda meli za kibiashara za utawala haramu wa Israel, Marekani na Uingereza ambazo zinalengwa na majeshi ya Yemen kulipiza kisasi jinai zinazotekelezwa na tawala hizo dhidi ya Wapalestina.

Mwishoni mwa juma, vikosi vya Marekani vilishambulia mji mkuu wa Yemen,  Sana'a kwa kupiga kituo cha kuhifadhia makombora na sehemu ya kuamrisha na kudhibiti, kulingana na taarifa ya Jumamosi kutoka CENTCOM.