UNICEF: Watoto 14500 wameuawa shahidi hadi sasa katika Ukanda wa Gaza
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i120510-unicef_watoto_14500_wameuawa_shahidi_hadi_sasa_katika_ukanda_wa_gaza
Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) limetangaza kuuawa shahidi watoto 14,500 wa Kipalestina huko Gaza.
(last modified 2024-12-23T10:47:47+00:00 )
Dec 23, 2024 10:47 UTC
  • UNICEF: Watoto 14500 wameuawa shahidi hadi sasa katika Ukanda wa Gaza

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) limetangaza kuuawa shahidi watoto 14,500 wa Kipalestina huko Gaza.

Taarifa ya UNICEF imeeleza kuwa, tangu kuanza vita na mashambulio ya Israel dhidi ya Ukanda wa Gazza Oktoba mwaka jana watoto 14,500 wa Kipalestinba wamethibitishwa kuuawa hadi sasa.

Wakati huo huo, Shirika la Misaada na Ajira kwa Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) pia limeripoti kuwa watoto 160 waliuawa shahidi katika mashambulizi ya Israel huko Gaza mwezi uliopita wa Novemba pekee.

Hayo yanajiri katika hali ambayo, ripoti mbalimbali za Mfuko wa Kuhudumia Watoto wa Umoja wa Mataifa (UNICEF) zimekuwa zikionya kuwa, hali ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza ni ya maafa matupu.

UNICEF inasema kuwa, watoto wanaojeruhiwa katika mashambulizi endelevu ya Israel hufikishwa hospitalini ambapo huduma za matibabu zimesimama. "Maisha ya watoto yapo hatarini si tu kwa sababu ya mashambulizi ya jeshi la Israel, bali pia kutokana na hali mbaya ya maisha wanayopitia", amesema msemaji wa Unicef.

Tangu Oktoba 7 mwaka jana utawala wa Israel umekuwa ukifanya mauaji makubwa ya kimbari dhidi raia wa Palestinan wasio na ulinzi wa Gaza na katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan huko Palestina kwa himaya na msaada wa pande zote za Marekani na baadhi ya nchi za Magharibi.