Utawala wa Kizayuni wakiri kuwa ndio uliomuua kigaidi Ismail Haniyeh
Waziri wa vita wa utawala wa Kizayuni kwa mara ya kwanza amekiri kwamba israel ndiyo iliyomuua kigaidi Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya HAMAS, Ismail Haniyeh mjini Tehran.
Ismail Haniyeh, Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS aliuliwa kigaidi akiwa pamoja na mlinzi wake mmoja alifajiri ya siku ya Jumatano ya tarehe 31 Julai 2024, mjini Tehran.
Israel Katz, waziri wa vita wa utawala wa Kizayuni, usiku wa kuamkia leo Jumanne ametoa vitisho kwa viongozi wa Yemen na kukiri kwa mara ya kwanza kwamba, Israel ndiyo iliyomuua Ismail Haniyeh, Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya HAMAS mjini Tehran.
Vilevile waziri huyo wa utawala wa kigaidi wa Israel ametoa vitisho vya kushambulia miundombinu na maeneo muhimu ya Yemen na kuwalenga pia viongozi wa nchi hiyo.
Wachambuzi wa mambo wanasema kuwa, matamshi hayo ya waziri wa vita wa Israel mbali na kuzidi kuthibitishwa kuwa utawala wa Kizayuni ni utawala wa kigaidi, yanaonesha pia hamaki, kuishiwa na kukata tamaa viongozi wa Israel kutokana na kushindwa kuzuia vipigo wanavyopokea kutoka kwa Kambi ya Muqawama vikiwemo vikosi vya Ulinzi vya Yemen na jinsi mifumo ya ulinzi ya Israel inavyoshindwa kuzuia makombora ya Yemen.