Yemen yashambulia Israel kwa kombora la pili la hypersonic
Jeshi la Yemen limetumia kombora la hypersonic kulenga ngome ya kijeshi ya utawala wa Kizayuni wa Israel ndani ya maeneo yanayokaliwa kwa mabavu ikiwa ni katika kuunga mkono Wapalestina wa Gaza.
Hilo nii shambulio la pili ndani ya siku mbili. Brigedia Jenerali Yahya Saree, msemaji wa Vikosi vya Wanajeshi wa Yemen, ametangaza Jumatano kwamba operesheni hiyo ilihusisha kombora la balestiki la Palestina-2, na kushambulia shabaha ya jeshi la Israel huko Tel Aviv.
Msemaji huyo wa Yemen amesisitiza kuwa shambulizi hilo la makombora lilikuwa sehemu ya awamu ya tano ya vita dhidi ya adui Muisraeli, na kwamba malengo yaliyotarajiwa yamefikiwa.
Amesema Vikosi vya Wanajeshi vya Yemen vitaendelea na operesheni zao, na vitashambulia vituo vyote vya Israel ndani ya maeneo yanayokaliwa kwa mabavu.
Aidha amebaini kuwa mashambulizi kama haya hayatakoma hadi pale utawala haramu wa Israel utakapositisha jinai zake dhidi ya Yemen.
Yemen imezidisha mashambulizi yake yanayoiunga mkono Palestina dhidi ya ngome za utawala ghasibu wa Israel katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu.
Mashambulizi ya hivi majuzi ni pamoja na shambulio la kombora la Jumanne kwenye eneo la kijeshi katika kitongoji cha kusini mwa Tel Aviv cha Jaffa, shambulio la Jumatatu kwenye eneo la Ashkelon, na shambulio la kombora la Jumamosi karibu na Tel Aviv. Idadi kubwa ya Wazayuni wameangamizwa na kujeruhiwa katika mashambulio hayo lakini utawala wa Kizayuni wa Isarel hautaki kutangaza kutangaza idadi rasmi kwani jambo hilo litaibua wahka miongoni mwa Wazayuni
Mashambulizi ya Yemen yanawafanya mamia ya maelfu ya walowezi kuingia kwenye mahandaki, huku jeshi la Israel likishindwa kutungua makombora hayo.
Majeshi ya Yemen yamejiimarisha kwa makombora ya masafa marefu, na ndege zisizo na rubani zenye uwezo wa kulenga shabaha hadi umbali wa kilomita 2,000.
Wananchi wa Yemen wametangaza uungaji mkono wao wa wazi kwa mapambano ya Palestina dhidi ya utawala ghasibu wa Israel tangu utawala huo ghasibu ulipoanzisha vita vyake vya mauaji ya kimbari dhidi ya Ghaza mnamo Oktoba 7, 2023.
Hadi sasa, Israel imewauwa Wapalestina wasiopungua 45,338, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, na kuwajeruhi wengine 107,764 huko Gaza.