Wanamgambo wa HTS Syria washambulia waandamanaji wanaolaani kuvunjiwa heshima eneo takatifu
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i120638-wanamgambo_wa_hts_syria_washambulia_waandamanaji_wanaolaani_kuvunjiwa_heshima_eneo_takatifu
Maandamano yamezuka kote nchini Syria kuhusiana na wanamgambo ambao wamevunjia heshima eneo takatifu la Waislamu wa madhehebu ya Alawi huko Aleppo, huku wanamgambo yenye silaha wa kundi la Hay'at Tahrir al-Sham (HTS) wakiwafyatulia risasi waandamanaji.
(last modified 2024-12-26T08:39:00+00:00 )
Dec 26, 2024 08:39 UTC
  • Wanamgambo wa HTS Syria washambulia waandamanaji wanaolaani kuvunjiwa heshima eneo takatifu

Maandamano yamezuka kote nchini Syria kuhusiana na wanamgambo ambao wamevunjia heshima eneo takatifu la Waislamu wa madhehebu ya Alawi huko Aleppo, huku wanamgambo yenye silaha wa kundi la Hay'at Tahrir al-Sham (HTS) wakiwafyatulia risasi waandamanaji.

Makumi kwa maelfu ya wananchi wamemmiinika mitaani huko Latakia, Tartus, Homs, Hama, na Qardaha tangu jana Jumatano, na kusababisha makabiliano makali baina hayo na wanamgambo ya HTS.

Waandamanaji walijitokeza baada ya kusambaa kwa video kwenye mitandao ya kijamii ikionyesha moto ndani ya kaburi la Abu Abdullah al-Hussein al-Khasibi huko Aleppo, huku watu wenye silaha wakiingia ndani na kuwaua walinzi wa kaburi hilo, tukio ambalo limelaaniwa vikali na jamii ya Alawi, ambao ni wachache nchini Syria.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka vyanzo vya ndani, maandamano hayo yalienea baada ya watu waliokuwa na silaha kuwafyatulia risasi waandamanaji huko Homs na kusababisha kifo cha mtu mmoja na wengine watano kujeruhiwa.

Vurugu hizo ziliendelea katika mji wa pwani wa Tartus, ambapo mapigano makali yalizuka kati ya wananchi wa wanamgambo wa wanachama wa "Wizara ya Mambo ya Ndani" ya utawala wa HTS.

Wizara mpya ya Mambo ya Ndani ya Syria imedai kwenye akaunti yake ya Telegram kwamba kanda za video za uharibifu wa kaburi hilo zilikuwa zimepitwa na wakati na zilihusiana na migogoro ya awali wakati wa kutwaliwa Aleppo mwishoni mwa Novemba.

Hata hivyo, matamshi haya hayajazima hasira za umma, kwani maelfu walikusanyika katika maandamano, wakitaka hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya wahusika wa mashambulizi dhidi ya turathi zao za kidini.

Maalawi wanazidi kuwa na wasiwasi juu ya uwezekano wa mashambulizi ya kulipiza kisasi dhidi ya jumuiya yao, kutokana na hadhi yao kama kikundi cha kidini cha wachache na uhusiano wao wa kihistoria na familia ya al-Assad, ambayo ni ya Kialawi, ikiwa ni pamoja na Rais aliyeondolewa madarakani, Bashar al-Assad.

Aidha, siku ya Jumanne, mamia ya waandamanaji waliandamana katika maeneo ya Kikristo ya Damascus kupinga kuchomwa kitendo cha moto kwa mti wa Krismasi karibu na Hama nchini Syria. 

Viongozi wapya wa Syria wameahidi mara kwa mara kuwawajibisha wale waliohusika na uchafuzi wa maeneo matakatifu ya kidini, wakidai kwamba wataheshimu imani na haki za madhehebu na dini zote.

Hali inasalia kuwa tete, huku kukiwa na hatari ya kutokea kwa mapigano zaidi huku hisia za kimadhehebu zikiendelea kukithiri sambamba na msukosuko wa kisiasa na mashinikizo kwa makundi ya wachache.