Hamas yaonya kuhusu sera za Israel za kujitanua
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i120786-hamas_yaonya_kuhusu_sera_za_israel_za_kujitanua
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas, imeonya kuhusu sera ya kujitanua ya utawala haramu wa Israel nchini Syria kufuatia kuanguka kwa Rais wa zamani wa nchi hiyo, Bashar al-Assad.
(last modified 2026-04-19T09:26:01+00:00 )
Dec 30, 2024 04:21 UTC
  • Hamas yaonya kuhusu sera za Israel za kujitanua

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas, imeonya kuhusu sera ya kujitanua ya utawala haramu wa Israel nchini Syria kufuatia kuanguka kwa Rais wa zamani wa nchi hiyo, Bashar al-Assad.

Hamas imeashiria maoni yaliyotolewa na waziri wa mawasiliano wa mrengo wa kulia wa Israel, Shlomo Karhi, kuhusu kufika hadi katika milango ya Damascus, ikionyesha nia za kimabavu za utawala huo kwa eneo hilo na watu wake.

Hamas imesema kwamba uvamizi wa gaidi Karhi katika viwanja vya Msikiti wa Al-Aqsa akiwa na walowezi wenye msimamo mkali na taarifa zake kuhusu kufikia Damascus zinathibitisha malengo ya kikoloni ya Israeli kwa ardhi za Waarabu. Harakati hiyo imetaka mataifa ya Kiarabu na Kiislamu kuungana dhidi ya sera za upanuzi za Israel na kukabiliana na mipango ya "utawala wa kifashisti".

Israeli imefanya mamia ya mashambulizi ya anga nchini Syria, ikilenga maeneo ya jeshi la nchi hiyo na miundombinu ya kiraia. Katika shambulio la hivi karibuni, watu wapatao 11 waliuawa katika mlipuko karibu na mji mkuu Damascus. Mlipuko huo katika ghala la silaha karibu na eneo la viwanda la Adra umeripotiwa kusababisha uharibifu mkubwa na majeruhi.