Wanajeshi wengine watano wa jeshi haramu la Israel wapelekwa jongomeo
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i120840-wanajeshi_wengine_watano_wa_jeshi_haramu_la_israel_wapelekwa_jongomeo
Wanajeshi wengine watano wa Israel wameangamizwa na wengine kadhaa kujeruhiwa kufuatia mashambulio ya roketi la wanamuqawama huko Beit Hanoun na Jabalia kaskazini mwa Ukanda wa Gaza.
(last modified 2024-12-31T08:32:45+00:00 )
Dec 31, 2024 08:32 UTC
  • Wanajeshi wengine watano wa jeshi haramu la Israel wapelekwa jongomeo

Wanajeshi wengine watano wa Israel wameangamizwa na wengine kadhaa kujeruhiwa kufuatia mashambulio ya roketi la wanamuqawama huko Beit Hanoun na Jabalia kaskazini mwa Ukanda wa Gaza.

Brigedi za Izzudin Qassam, Tawi la Kijeshi la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS zimetangaza kuwa, zimevurumisha maroketi na kuwaangamiza wanajeshi wa utawala haranmu wa Israel.

Kabla ya hapo pia, Brigedi za Izzudin Qassam, Tawi la Kijeshi la Harakati ya Mapambano ya Palestina HAMAS zilikuwa zimesambaza mkanda wa video unaoonesha jinsi wanamapambano hao walivyoteketeza kifaru cha Merkava cha jeshi vamizi la Israel.

Makundi ya muqawama ya Wapalestina yanaendelea na operesheni zao dhidi ya jeshi katili la Israel kwa kuvurumisha makombora zaidi kwenye ngome za utawala wa Israel katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu.

Kulingana na takwimu za jeshi, idadi ya askari wake walioangamizwa tangu kuanza kwa vita vya mauaji ya kimbari huko Gaza, Oktoba 7, 2023, sasa imeongezeka hadi wanajeshi karibu 900.

Takwimu hizo zinajumuisha wanajeshi waliouawa katika Ukanda wa Gaza, Ukingo wa Magharibi, Lebanon na ndani ya Israel.

Wapigania ukombozi wa Palestina wanasisitiza kwamba hasara ya vikosi vya utawala haramu wa Israel ni kubwa zaidi kuliko inayotangazwa.