Askari wengi wa Israel wanajiua kutokana na vita Gaza
Jeshi la Israel limeripoti ongezeko kubwa la vifo vya kujiua miongoni mwa wanajeshi tangu kuanzishwa kwa kampeni ya mauaji ya kimbari dhidi ya Ukanda wa Gaza uliozingirwa
Katika taarifa iliyotolewa Alhamisi, jeshi limesema kuwa angalau wanajeshi 28 wa Israel wamejiua tangu Oktoba 2023.
Takwimu hizi zinaonyesha ongezeko kubwa kutoka miaka iliyopita. Mwaka 2022, jeshi la Israel liliripoti vifo 14 vilivyoshukiwa kuwa vya kujiua, na mwaka 2021 idadi ilikuwa 11.
Kwa ujumla, idadi ya vifo vya wanajeshi katili wa Isarel mwaka 2023-2024 ni kubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa katika miongo kadhaa kutokana na vita.
Kulingana na takwimu zilizotolewa na jeshi hilo, angalau wanajeshi 891 wa Israel wameuawa na wengine 5,569 wamejeruhiwa tangu kuanza kwa vita dhidi ya Gaza.
Jeshi lilisema kuwa wanajeshi 363 waliuawa mwaka 2024, idadi iliyo chini kutoka wanajeshi 558 waliouawa mwaka 2023. Mwaka 2022, wanajeshi 44 wa Israel waliuawa.
Kulingana na takwimu hizo, vifo vya kujiua sasa ni sababu ya pili ya vifo ndani ya jeshi la Israeli, nyuma ya vifo vitani.
Vikundi vya muqawama vya Wapalestina vinasema kuwa idadi ya vifo ni kubwa zaidi kwani utawala wa Israel unadumisha usiri mkali na hauachi taarifa za kweli za vifo vya wanajeshi wake kwa hofu ya hasira ya umma kuhusu vita.
Katika miezi ya hivi karibuni, Wapalestina wameongeza operesheni zao za muqawama wakikabiliana na mashambulizi ya Israel yaliyoongezeka kaskazini mwa Gaza na sehemu nyingine za ukanda huo uliozingirwa.
Utawala haramu wa Israel ulianzisha vita vya mauaji ya kimbari dhidi ya Gaza mnamo Oktoba 7, 2023 na hadi sasa jeshi katili la utawala huo limewaua Wapalestina 45,553 wengi wao wakiwa wanawake na watoto na kuwajeruhi wengine 108,379.