Operesheni za Mhimili wa Muqawama dhidi ya utawala ghasibu wa Israel
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i120950-operesheni_za_mhimili_wa_muqawama_dhidi_ya_utawala_ghasibu_wa_israel
Huku kukiwa na vita vya mauaji ya kimbari ya Israel yanayoungwa mkono na mataifa ya Magharibi  hasa Marekani dhidi ya Gaza, ambayo yamesababisha vifo vya takriban Wapalestina 45,600 hadi sasa, makundi ya muqawama huko Palestina na katika eneo zima la Asia Magharibi yanaendelea na operesheni zao dhidi ya utawala wa Israel na waungaji mkono wake wa Magharibi.
(last modified 2026-04-19T09:26:01+00:00 )
Jan 03, 2025 04:04 UTC
  • Operesheni za Mhimili wa Muqawama dhidi ya utawala ghasibu wa Israel

Huku kukiwa na vita vya mauaji ya kimbari ya Israel yanayoungwa mkono na mataifa ya Magharibi  hasa Marekani dhidi ya Gaza, ambayo yamesababisha vifo vya takriban Wapalestina 45,600 hadi sasa, makundi ya muqawama huko Palestina na katika eneo zima la Asia Magharibi yanaendelea na operesheni zao dhidi ya utawala wa Israel na waungaji mkono wake wa Magharibi.

Operesheni kuu za makundi ya muqawama ya Palestina na kikanda siku ya Alhamisi, Januari 2, ni kama ifuatavyoWapiganaji wa tawi la kijeshi la Hamas, Brigedi za Ezzedin Al-Qassam 'walilenga makazi ya walowezi wa Kizayuni ya Netivot kwa idadi kubwa ya maroketi aina ya "Q18".

Nao wapiganaji wa tawi la  Kijeshi la Harakati ya Jihad Islamu, Brigedi za Al-Quds, walilenga makazi ya walowezi wa Kizayuni Holit kwenye karibu na Gaza kwa safu ya makombora "107".

Katika operesheni ya pamoja na makundi mengine ya muqawama, wapiganaji wa Brigedi za Mashahidi wa Al-Aqsa, walishambulia mikusanyiko ya wanajeshi wa Israel mashariki mwa eneo la Malka, karibu na mji wa Gaza, kwa kutumia makombora.

Kwingineko, Kikosi cha Al-Mujahideen, katika Ukingo wa Magharibi kimelenga tingatinga za jeshi la Kizayuni la Israel katika kambi ya Tulkarem, iliyoko katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu.

Wakati huo huo, mapema Ijumaa asubuhi Yemen imefanya mashambulizi ya kombora dhidi ya ngome za utawala haramu Israel ikiwa ni kuonyesha mshikamano na Wapalestina.

Ving'ora vya mashambulizi ya anga vilisikika katikati na kusini mwa maeneo yanayokaliwa kwa mabavu (Israel) mapema Ijumaa wakati kombora lilipovuka hadi katika maeneo hayo..

Jeshi la Israel lilidai kuwa kombora hilo "lilizuiliwa", likinukuu ripoti kuhusu makombora kutoka kwenye eneo la Modi'in. Wakati mwingi Israel hutangaza imetungua makombora ili kutuliza Wazayuni waliojaa khofu.

Taarifa zinasema walowezi wa Kizayuni wameuawa au kujeruhiwa kwa wingi katika operesheni hizo lakini utawala wa Kizayuni wa Israel unatumia kila mbinu kubana habari hizo.

Tangu kuanza kwa vita vya mauaji ya kimbari ya Israel dhidi ya Wapalestina aktika Ukanda wa Gaza mnamo Oktoba 2023, vikosi vya Yemen vimekuwa vikitekeleza operesheni nyingi za kuwaunga mkono Wapalestina wa Gaza waliokumbwa na vita, na kulenga ngome za kijeshi na kibiashara za Israel.