Wanajeshi 3 wa Israel waangamizwa kaskazini mwa Ukanda wa Gaza
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i121386-wanajeshi_3_wa_israel_waangamizwa_kaskazini_mwa_ukanda_wa_gaza
Wanajeshi 3 wa Kizayuni wameangamizwa katika shambulizi la kuvizia la wanamuqawama dhidi ya Wazayuni kaskazini mwa Gaza.
(last modified 2025-01-13T07:41:57+00:00 )
Jan 13, 2025 07:41 UTC
  • Wanajeshi 3 wa Israel waangamizwa kaskazini mwa Ukanda wa Gaza

Wanajeshi 3 wa Kizayuni wameangamizwa katika shambulizi la kuvizia la wanamuqawama dhidi ya Wazayuni kaskazini mwa Gaza.

Katika shambulio hilo la kuvizia dhidi ya adui Mzayuni, wanamapabmano wa Palestina walilipua jengo moja kaskazini mwa Ukanda wa Gaza ambapo kundi la askari jeshi wa Israel kutoka brigedi ya Nahal walikuwa hapo. 

Duru za habari za Kizayuni zimeripoti kuwa wanajeshi watatu wa jeshi la Israel wameuawa na kumi wamejeruhiwa. 

Wakati huo huo, ndege za kivita za jeshi la utawala wa Israel zilielekea katika eneo la tukio na kuwachukua askari majeruhi. 

Jeshi la utawala wa Kizayuni jana asubuhi pia lilitangaza kuwa wanajeshi wake wanne kutoka brigedi ya Nahal wameuawa na watano kujeruhiwa.

Duru za Kizayuni zimearifu kuwa, wanajeshi wa utawala huo wameangamizwa katika eneo la Bait Hanoun huko kaskazini mwa Ukanda wa Gaza baada ya bomu kuripuka miongoni mwa kundi la wanajeshi wa utawala huo. 

Kanali ya 12 ya Televisheni ya utawala wa Kizayuni pia ilitangaza kuwa, shambulio la Bait Hanoun lilikuwa la kuvizia ambapo kwanza bomu la kutegw aardhini liliripuka, na kisha wanajeshi wa walishambuliwa.