Uchunguzi wa maoni: Asilimia 63 ya Wazayuni wanataka Netanyahu ajiuzulu
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i121898-uchunguzi_wa_maoni_asilimia_63_ya_wazayuni_wanataka_netanyahu_ajiuzulu
Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala haramu wa Israel ameendelea kuandamwa na mashinikizo yanayomtaka ajiuzulu hasa baada ya Israel kushindwa kufikia malengo yake katika vita vya Gaza.
(last modified 2026-06-23T03:13:58+00:00 )
Jan 25, 2025 22:52 UTC
  • Uchunguzi wa maoni: Asilimia 63 ya Wazayuni wanataka Netanyahu ajiuzulu

Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala haramu wa Israel ameendelea kuandamwa na mashinikizo yanayomtaka ajiuzulu hasa baada ya Israel kushindwa kufikia malengo yake katika vita vya Gaza.

Matokeo ya uchunguzi yanaonesha kuwa, asilimia 63 ya Wazayuni wanataka kujiuzulu Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na wanaamini kwamba hapaswi kubaki madarakani.

Kwa mujibu wa Channel 12 ya utawala wa Kizayuni, kwa mujibu wa uchunguzi wa kanali hii, ni asilimia 27 tu ya Wazayuni ndio wanaopinga kujiuzulu Netanyahu.

Hivi karibuni, Kituo cha Habari cha Palestina pia kilitangaza kuwa, kwa mujibu wa uchunguzi wa gazeti la Kizayuni la Ma'ariv, asilimia 62 ya Wazayuni walisema kuwa Netanyahu ndiye anayebeba dhima ya pigo la kiusalama la Oktoba 7.

Jeshi na baraza la mawaziri la utawala wa Kizayuni wamekabiliwa na hali mbaya kutokana na matokeo ya usitishaji vita katika Ukanda wa Gaza.

Kujiuzulu kwa makamanda wa jeshi la utawala wa Kizayuni na hatua za wapinzani za kutaka kumuondoa madarakani Waziri Mkuu wa utawala huo Benjamin Netanyahu katika siku za hivi karibuni yamekuwa matokeo ya kimsingi ya usitishaji vita katika Ukanda wa Gaza.

Harakati za wapinzani wa Baraza la Mawaziri la Benjamin Netanyahu pia zimeongezeka na kutaka waziri mkuu wa utawala huo na wajumbe wake wa baraza la mawaziri kujiuzulu, pamoja na kuundwa kwa kamati rasmi ya uchunguzi kuchunguza kushindwa kwa Oktoba 7, 2023.