Hamas yatangaza kuuawa shahidi kamanda wake wa kijeshi, Mohammed Deif
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i122124-hamas_yatangaza_kuuawa_shahidi_kamanda_wake_wa_kijeshi_mohammed_deif
Brigedi za Hizzuddin al Qassam , Tawi la Kijeshi la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS, zimethitibisha habari kuuawa shahidi makamanda wake kadhaa katika mashambulizi ya kikatili ya Israel kwenye eneo lililozingirwa kila upande la Ghaza, akiwemo mkuu wake wa majeshi, Mohammed Deif.
(last modified 2026-05-20T03:07:53+00:00 )
Jan 31, 2025 03:00 UTC
  • Hamas yatangaza kuuawa shahidi kamanda wake wa kijeshi, Mohammed Deif

Brigedi za Hizzuddin al Qassam , Tawi la Kijeshi la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS, zimethitibisha habari kuuawa shahidi makamanda wake kadhaa katika mashambulizi ya kikatili ya Israel kwenye eneo lililozingirwa kila upande la Ghaza, akiwemo mkuu wake wa majeshi, Mohammed Deif.

Mkuu wa Brigedi za al-Qassam Abu Obeida jana Alkhamisi alithibitisha kuuawa shahidi pia Naibu Kamanda wa kijeshi wa HAMAS, Marwan Issa katika mapigano na Wazayuni.

Makamanda wengine waliouawa shahidi katika vita hivyo ni pamoja na Ghazi Abu Tama’a, kamanda wa silaha na huduma za kivita, Raed Thabet, kamanda wa wafanyakazi na mkuu wa kitengo cha vifaa na Rafeh Salama, kamanda wa Brigedi ya Khan Younis.

Kamanda Mohammed Deif

 

Ahmed al-Ghandour, kamanda wa Brigedi ya Kaskazini na Ayman Nofal, kamanda wa Brigedi ya Katikatika mwa Ghaza, ni makamanda wengine wa HAMAS waliouawa shahidi katika mapambano na Israel. 

Mohammad 'Abu Khaled' Deif, aliyekuwa maarufu kwa kutoonekana kirahisi, alinusurika kuuawa shahidi kwa uchache katika majaribio saba wakati wa maisha yake ya mapambano na utawala wa kigaidi wa Israel. Alikuwa mtu muhimu katika kuandaa operesheni za kijeshi dhidi ya Israel.

Huko nyuma vyombo vya habari vilitangaza habari ya kuuawa shahidi Deif, lakini tangazo la jana Alkhamisi la Abu Obeida ni uthibitisho wa kwanza rasmi kutoka kwa Hamas juu ya kuuawa shahidi kamanda wake huyo shujaa. 

Abu Obeida amesema kuwa tangazo lao hilo lilikuwa linasubiri kukamilishwa taratibu muhimu na kushughulikia masuala ya kiusalama wakati wa vita. 

Vilevile amesema kuwa, makumi ya makamanda wengine wameziba nafasi za makamanda hao waliouawa shahidi na ndio maana huoni kutetereka HAMAS wala Tawi lake la Kijeshi yaani Brigedi za Izzuddin al Qassam.