Marekani, chanzo cha fitina katika Ulimwengu wa Kiislamu
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i12220-marekani_chanzo_cha_fitina_katika_ulimwengu_wa_kiislamu
Kiongozi wa harakati ya Ansarullah ya Yemen amesisitiza kuwa chanzo cha fitina zote na migogoro ya hivi karibuni katika Ulimwengu wa Kiislamu ni hatua za wazi na za siri za Marekani na waitifaki wake.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Jul 29, 2016 16:33 UTC
  • Marekani, chanzo cha fitina katika Ulimwengu wa Kiislamu

Kiongozi wa harakati ya Ansarullah ya Yemen amesisitiza kuwa chanzo cha fitina zote na migogoro ya hivi karibuni katika Ulimwengu wa Kiislamu ni hatua za wazi na za siri za Marekani na waitifaki wake.

Abdulmaliki Badruddin al Houth Kiongozi wa harakati ya Ansarullah ya Yemen amesema kuwa Marekani imechukua misimamo ya kiuhasama dhidi ya Ulimwengu wa Kiislamu na kwamba chanzo cha fitina zote na migogoro ya mwaka huu katika Ulimwengu wa Kiislamu ni hatua na mienendo ya waziwazi na ya siri ya Marekani na nchi waitifaki wake. 

Kiongozi wa harakati ya Ansarullah ya Yemen ameeleza kuwa Marekani imejawa na tamaa kubwa na kwa msingi huo inaendelea kuzikandamiza nchi nyingine. Amesema Marekani inafanya kila iwezalo ili kudhibiti kikamilifu na moja kwa moja utajiri wa Umma wa Kiislamu. 

Abdulmalik Badruddin ameongeza kuwa Umma wa Kiislamu umelengwa na njama kubwa zilizoratibiwa na Marekani na Israel, huku tawala hizo zikifaidika na migogoro iliyopo katika Umma huo. Badruddin al Houthi amesema historia inaonyesha kuwa Marekani na Israel zimekuwa zikifanya kila ziwezalo kuzusha vita katika Ulimwengu wa Kiislamu; na kwamba tawala hizo hazijajiepusha na jitihada yoyote ya kutoa pigo kwa Umma wa Kiislamu.

Saudia na Israel

Amesema katika eneo hili la Mashariki ya Kati kuna serikalil vibaraka wa Marekani na Israel ambazo ziko tayari  kufanya lolote litakaloagizwa na Marekani.

Marekani na Israel, chanzo cha fitina na migogoro katika Ulimwengu wa Kiislamu