Jumuiya ya Wanazuoni Yemen: Jihadi dhidi ya uvamizi wa Marekani ni wajibu
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i125528-jumuiya_ya_wanazuoni_yemen_jihadi_dhidi_ya_uvamizi_wa_marekani_ni_wajibu
Jumuiya ya Maulamaa wa Yemen imesisitiza haja ya uhamasishaji wa jihadi, utayari wa vita, na utayari wa kujitolea katika kukabiliana na uvamizi wa Marekani.
(last modified 2025-04-23T07:39:31+00:00 )
Apr 23, 2025 07:39 UTC
  • Jumuiya ya Wanazuoni Yemen: Jihadi dhidi ya uvamizi wa Marekani ni wajibu

Jumuiya ya Maulamaa wa Yemen imesisitiza haja ya uhamasishaji wa jihadi, utayari wa vita, na utayari wa kujitolea katika kukabiliana na uvamizi wa Marekani.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Al-Ahd la Lebanon, Jumuiya ya Wanazuoni wa Yemen imetoa taarifa hiyo na kusisitiza ulazima wa kukabiliana na hujuma za Marekani dhidi ya Yemen na kuongeza kuwa: "Wajibu wa kidini, kisheria na kijihadi wa majeshi ya Kiarabu kusaidia na kuunga mkono Gaza unazidi kuwa muhimu na mgumu."

Ikiashiria uhalali wa silaha za muqawama na kuwa haramu mjadala wowote wa wazo la kuwapokonya silaha wapiganaji huko Palestina, Lebanon, Yemen, na kadhalika taarifa ya jumuiya hiyo imeeleza: Kuunga mkono wazo la kujadili upokonyaji silaha muqawama ni usaliti kwa Mwenyezi Mungu, Mtume, na waumini, na huduma mbaya katika uaminifu wa wazi kwa Israel na Marekani.

Jumuiya ya Wanazuoni wa Yemen pia imesisitiza haja ya uhamasishaji wa uumma na utayari watu wa Yemen kwa ajili ya mapambano dhidi ya mvamizi Marekani na washirika wake.

Marekani imezidisha mashambulizi yake mabaya dhidi ya nchi hiyo maskini tangu mwezi uliopita, kwa amri ya moja kwa moja ya Rais Donald Trump.

Serikali ya Yemen imeapa kwamba, uhalifu huu hautapita bila kujibiwa, ikisisitiza kuwa Marekani haitaambulia chochote ila kushindwa na kufeli kwa fedheha. Jeshi la Marekani limedai kuwa bandari hiyo ni chanzo cha mafuta kwa Harakati ya Muqawama ya Ansarullah.

Vikosi vya Jeshi la Yemen vimeendesha msururu wa operesheni kulipiza kisasi kutokana na mashambulizi yanayoendelea ya Marekani katika nchi hiyo ya Kiarabu, vikishambulia ngome muhimu za Isarel katika ardhi zinazikaliwa kwa mabavu pamoja na meli za kivita za Marekani katika Bahari Nyekundu ya Kaskazini na Bahari ya Arabia.