Ahmadian: Iran na Pakistan hazitaruhusu usalama wa kikanda kutumiwa vibaya na maadui
(last modified Tue, 20 May 2025 06:23:19 GMT )
May 20, 2025 06:23 UTC
  • Ahmadian: Iran na Pakistan hazitaruhusu usalama wa kikanda kutumiwa vibaya na maadui

Afisa usalama wa ngazi ya juu wa Iran amesema kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Pakistan kamwe hazitaruhusu usalama wa kanda hii kutumiwa vibaya na maadui.

Ali Akbar Ahmadian Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran (SNSC) amebainisha haya katika mazungumzo ya simu na Mshauri wa Usalama wa Taifa wa Pakistan Luteni Jenerali Muhammad Asim Malik. 

Ahmadian amesema, Iran inatilia maanani sana kuimarisha ushirikiano na Pakistan, hususan katika nyanja za kisiasa, kiuchumi na kiusalama.

Amesema, mataifa haya mawili jirani yamedhamiria kuimarisha usalama wa mipaka yao ya pamoja na kupambana na ugaidi; na hazitaruhusu usalama wa watu wa kanda hii kuchezewa na maadui. 

Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran ametilia mkazo kwamba ushirikiano wa Tehran na Pakistan ni kwa maslahi ya usalama wa eneo na kwamba nchi yake imedhamiria kwa dhati kuimarisha ushirikiano wa pande mbili na Iran. 

Katika mazungumzo hayo ya simu ya jana Jumatatu, Asim Malik amesifu mchangao athirifu wa Iran katika eneo na kusema Islamabad iko tayari kukuza uhusiano na Tehran katika nyanja za kisiasa, kiusalama na kijamii.