Sep 03, 2016 06:57 UTC
  • Utawala wa Aal Khalifa umeshindwa kudiriki ujumbe wa mwamko wa Wabahrain

Sheikh Issa Qassim mwanazuoni wa ngazi za juu wa Kiislamu nchini Bahrain ametoa ujumbe na kuuonya vikali ukoo wa Aal Khalifa unaotawala nchini humo kuhusu sera zake za kuzidisha mashinikizo dhidi ya Waislamu wa madhehebu ya Shia wanaodhulumiwa nchini humo.

Sheikh Qassim pamoja na mwanazuoni mwingine maarufu wa Kishia Sheikh Abdullah al-Ghureifi wametoa taarifa na kuuonya utawala wa ukoo wa Aal Khalifa kuhusu kuzuia sala ya Ijumaa na kuendelea kuwakandamiza Mashia.

Wamesema Sala ya Ijumaa ni nukta ya pamoja ya madhehebu zote za Kiislamu na hakuna  dhehebu lolote la Kiislamu linalopinga Sala hiyo.

Wanazuoni hao wamesema utawala wa Aal Khalifa haujaweza kutambua utambulisho na ujumbe wa wazi wa mwamko wa amani wa watu wa Bahrain. Sheikh Qassim na Sheikh al Ghureifi wamesema utawala wa Bahrain unatumia mkono wa chuma kuwakandamiza wananchi hadi kufikia kiwango cha kutumia wanajeshi katili wa Saudia ambao sasa wanaikalia kwa mabavu nchi hiyo.

 

Bahrain imekuwa ikishuhudia maandamano ya amani ya wananchi dhidi ya utawala wa Aal Khalifa tangu mwezi Februari mwaka 2011. Wananchi wa Bahrain wanataka marekebisho ya kisaisa, wanadai ikuwa huru, wanataka kutekelezwa uadilifu, kukomeshwa vitendo vya ubaguzi na kuingia madarakani serikali iliyochaguliwa kwa njia ya kidemokrasia, hata hivyo utawala wa Aal Khalifa siku zote umekuwa ukiwakandamiza raia, kuwaua na kuzuia maandamano ya amani ya raia hao.

Tags