Sep 12, 2016 02:30 UTC
  • Utiwaji mbaroni wa kidhalimu waongezeka Bahrain

Kituo cha Haki za Binadamu cha nchini Bahrain kimebainisha wasiwasi wake kuhusu kuongezeka utiwaji mbaroni raia kidhulma nchini humo.

Inas Aun Afisa Anayehusika na Nyaraka wa KItuo cha Haki za Binadamu huko Bahrain amesema kuwa utiaji mbaroni raia kidhumla uliofanywa na utawala wa nchi hiyo mwaka huu umeongezeka sana ikilinganishwa na miaka iliyopita, kwa kadiri kwamba hadi kufikia sasa watu waliotiwa mbaroni nchini humo wanakaribia elfu moja.

Inas Aun amesisitiza kuwa idadi ya wafungwa wa kisiasa pia imeongezeka na kufikia 989 kuanzia tarehe Mosi Januari mwaka huu hadi Agosti 31, ambapo kati yao kuna wafungwa watoto 147 na wanawake 17.

Afisa huyo wa Kituo cha Haki za Binadamu cha Bahrain ameongeza kuwa, madai yanayotolewa na utawala wa Aal Khalifa kuhusu kuunda kamati ya kutafuta ukweli ni uwongo mtupu na kueleza kuwa utiaji mbaroni huo unafanyika kwa kupuuza haki za raia kama ilivyobainishwa ndani ya katiba; kiasi kwamba mtu yoyote anayeonekana kutoa maoni au mtazamo unaoupinga utawala wa Aal Khalifa hutiwa mbaroni na kufungwa jela.

Inas Aun ametaka kuachiwa huru wafungwa wa kisiasa wa Bahrain na wafungwa hao kunufaika na haki zao za kiraia kwa mujibu wa katiba ya nchi hiyo. 

Maandamano ya kutaka kuachiwa huru wafungwa wa kisiasa huko Bahrain

 

 

 

Tags