Saudi Arabia kufungua kituo cha kijeshi Djibouti
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i20734-saudi_arabia_kufungua_kituo_cha_kijeshi_djibouti
Katika kile kinachoonekana ni mkakati wa kupanua satua na uwepo wake wa kijeshi katika nchi za Afrika, utawala wa Saudi Arabia unapania kufungua kituo cha kijeshi nchini Djibouti.
(last modified 2026-01-02T07:57:23+00:00 )
Dec 04, 2016 14:59 UTC
  • Saudi Arabia kufungua kituo cha kijeshi Djibouti

Katika kile kinachoonekana ni mkakati wa kupanua satua na uwepo wake wa kijeshi katika nchi za Afrika, utawala wa Saudi Arabia unapania kufungua kituo cha kijeshi nchini Djibouti.

Katika mahojiano na gazeti la Saudia la Sharq al-Ausat, Mahmoud Ali Youssouf, Waziri wa Mambo ya Nje wa Djibouti amesema nchi hiyo ndogo ya Afrika inakaribisha mpango huo wa utawala wa Riyadh wa kuanzisha kituo chake cha kijeshi katika ardhi ya nchi hiyo.

Amesema mazungumzo kuhusu kadhia hiyo yameshafanyika na kinachosubiriwa ni kutiwa saini hati ya makubaliano kati ya nchi hizo mbili hivi karibuni.

Askari wa Saudia

Nchi hiyo maskini ya Pembe ya Afrika imekuwa ikifuata kibubusa sera za Saudia, ili ifaidike na misaada na ruzuku kutoka utawala wa kifalme wa Aal-Saud.

Itakumbukwa kuwa, tarehe 6 Januari mwaka huu, Waziri wa Mambo ya Nje wa Djibouti alisema kuwa, nchi hiyo ndogo ya Pembe ya Afrika imeamua kukata uhusiano wake na Iran ili kufuata siasa za Saudi Arabia. 

Djibouti inaruhusu utawala wa Riyadh uanzishe kambi ya kijeshi katika ardhi yake katika hali ambayo, Saudia imekuwa ikitekeleza mauaji na jinai za kutisha dhidi ya wananchi wa nchi jirani ya Yemen, tokea Machi mwaka jana, ambapo Wayemen zaidi ya 11 elfu wasio na hatia wameuawa, mbali na kuharibiwa asilimia kubwa ya miundomsingi ya nchi hiyo ya Kiarabu.