UN: Machafuko yameua watu 670 nchini Iraq mwezi Februari
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i2284-un_machafuko_yameua_watu_670_nchini_iraq_mwezi_februari
Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa watu 670 wameuawa katika machafuko na vitendo vya kigaidi nchini Iraq kwenye mwezi uliopita wa Februari pekee.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 02, 2016 04:15 UTC
  • UN: Machafuko yameua watu 670 nchini Iraq mwezi Februari

Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa watu 670 wameuawa katika machafuko na vitendo vya kigaidi nchini Iraq kwenye mwezi uliopita wa Februari pekee.

Takwimu zilizotolewa na ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq (UNAMI) zimeonesha kuwa Wairaqi 670 wameuawa mwezi uliopita wa Februari na wengine 1290 kujeruhiwa katika mashambulizi ya kigaidi. Takwimu hizo zimeonesha kuwa, raia waliouawa ni 410 na wengine 1050 wamejeruhiwa. Imesema 260 kati ya waliouawa walikuwa askari usalama.

Taarifa ya UNAMI imesema kuwa, udadi kubwa ya mauaji hayo ya kigaidi ilitokea katika mji mkuu wa Iraq, Baghdad ambako raia 277 na wengine 838 walijeruhiwa.

Mjumbe Maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq, Jan Kubis ameeleza kusikitishwa na mauaji ya raia nchini hiyo yanayosababishwa na machafuko na mashambulizi ya kigaidi. Jan Kubis ameongeza kuwa raia wa kawaida wanaunda thuluthi mbili ya wahanga na mauaji ya kigaidi yaliyotokea mwezi Februari nchini Iraq.

Umoja wa Mataifa umesema Wairaqi 849 waliuawa nchini Iraq mwezi wa Januari mwaka huu na wengine 1450 kujeruhuwa.

Kundi la kigaidi la Daesh linaloungwa mkono na Saudi Arabia, Uturuki na Qatar limekuwa likifanya mashambulizi ya mara kwa mara katika maeneo ya umma na kuua idadi kubwa ya raia wasio na hatia nchini Iraq.