Jan 31, 2017 04:10 UTC
  • UN: Saudi Arabia imetenda jinai kubwa za kivita nchini Yemen

Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, Saudi Arabia imefanya jinai za kivita katika mashambulizi yake ya kijeshi nchini Yemen.

Ripoti iliyotolewa na Umoja wa Mataifa imesema kuwa, rais 300 wa Yemen wameuawa katika mashambulizi 10 tu yaliyofanywa na ndege za kivita za Saudi Arabia baina ya mwezi Machi na Oktoba mwaka 2016. 

Ripoti hiyo ya Umoja wa Mataifa imeongeza kuwa, hakuna ushahidi wowote unaoonesha kwamba mashambulizi hayo yalilenga maeneo ya kijeshi. 

Umoja wa Mataifa pia umeitaka Saudi Arabia ikome kukiuka sheria za kimataifa. 

Raia wa Yemen wanaendelea kuuawa ovyo

Awali katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon alikemea mashambulizi ya Saudi Arabia dhidi ya raia wa Yemen na kutoa wito wa kufanyika uchunguzi usiopendelea upande wowote kuhusu mashambulizi ya nchi hiyo dhidi ya watu wa Yemen na kuwafikisha mahakamani wahusika. 

Ripoti za Umoja wa Mataifa zinaonesha kuwa, zaidi ya raia elfu 11 wa Yemen wameuawa katika mashambulizi ya Sauidi Arabia na washirika wake dhidi ya nchi hiyo ya Waislamu.  

Tags