Mar 18, 2017 02:50 UTC
  • Syria: Shambulizi la Israel ni jaribio la kuwapa motisha magaidi

Wizara ya Mambo ya Nje ya Syria imemwandikia barua Karibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu shambulizi lililofanywa na utawala haramu wa Israel katika ardhi ya nchi hiyo na kusema ni ukiukaji wa sheria za kimataifa na mamlaka ya kujitawala ya Syria.

Barua za serikali ya Syria kwa taasisi hizo mbili imesema kuwa shambulizi lililofanywa na Israel mapema jana (Ijumaa) ni jaribio la kutaka kuinua mori na moyo ulioporomoka wa makundi ya kigaidi baada ya kupata kipigo kutoka kwa jeshi la serikali ya Syria na waitifaki wake.

Ujumbe huo omeongeza kuwa, sababu zinazotolewa na utawala haramu wa Israel kwa ajili ya kufanya mashambulizi hayo ni upotoshaji unaotumiwa mara zote utawala huo unaposhindwa kuhalalisha uvamizi na kitendo chake cha kuendelea kuikalia kwa mabavu milima ya Golan na ardhi ya Palestina.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Syria imemtaka Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Mwenyekiti wa Baraza Kuu la umoja huo  kulaani shambulizi hilo la Israel. Vilevile Syria imeitaka Israel kukomesha uungaji mkono wake kwa makundi ya kigaidi nchini Syria na kuheshimu maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa yanayozitaka pande zote kupambana na ugaidi na vilevile azimio nambari 2253 linaloitaka Israel kuondoka katika miinuko ya Golani ya Syria inayokaliwa kwa mabavu.

Ndege za kivita za Israel

Jeshi la Israel limetangaza kuwa ndege nne za kivita za Israel ziliingia katika anga ya nchi hiyo mapema Ijumaa na kwamba jeshi la nchi hiyo limefanikiwa kutungua moja kati ya ndege hizo.     

Tags