Makumi ya makuhani wa Kizayuni wadhalilisha watu kijinsia, watiwa mbaroni
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i27032-makumi_ya_makuhani_wa_kizayuni_wadhalilisha_watu_kijinsia_watiwa_mbaroni
Zaidi ya makuhani 20 wa Kizayuni katika ardhi za Palestina zilizovamiwa na kuanza kukaliwa kwa mabavu na utawala wa Kizayuni mwaka 1948 wametiwa mbaroni kwa kosa la kuwadhalilisha watu kijinsia.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Mar 30, 2017 02:32 UTC
  • Makumi ya makuhani wa Kizayuni wadhalilisha watu kijinsia, watiwa mbaroni

Zaidi ya makuhani 20 wa Kizayuni katika ardhi za Palestina zilizovamiwa na kuanza kukaliwa kwa mabavu na utawala wa Kizayuni mwaka 1948 wametiwa mbaroni kwa kosa la kuwadhalilisha watu kijinsia.

Shirika la habari la Buratha la nchini Iraq limeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, polisi wa Israel wamewatia mbaroni makuhani 22 wa Kiyahudi kwa tuhuma za kuwadhalilisha kijinsia wanawake, wavulana na watoto wadogo katika mji wa Quds, na kwenye eneo la Beit Shemesh, magharibi mwa Baytul Muqaddas na vile vile katika eneo la Bani Burak, karibu na Tel Aviv na kwenye kitongoji cha Beitar katika Ukingo wa Magharibi mwa Mto Jordan.

Polisi ya Israel imetangaza kuwa, makuhani hao wa Kiyahudi ambao wamefanya uhalifu huo katika kipindi cha miaka miwili iliyopita wana umri wa kati ya miaka 20 hadi 60.

Bendera ya utawala wa Kizayuni wa Israel

 

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, baadhi ya makuhani wa Kizayuni walikuwa na taarifa kamili kuhusu uhalifu wa makuhani hao, lakini walificha na hawakuripoti polisi.

Asilimia 10 ya wakazi wa utawala wa Kizayuni wa Israel wanasoma masomo ya Taurati katika shule za kidini za Israel.

Ufisadi wa kiuchumi na kijinsia umeigubika jamii ya Israel na hasa kati ya wanasiasa na makamanda wa ngazi za juu jeshini kiasi kwamba hivi sasa Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni anakabiliwa na tuhuma kubwa za ufisadi wa kisiasa na kiuchumi.