Apr 03, 2017 13:57 UTC
  • Mfalme wa Bahrain aafiki kuhukumiwa raia katika mahakama za kijeshi

Mfalme wa Bahrain leo Jumatatu amesaini sheria ya kuifanyia marekebisho katiba ili kuzipatia mamlaka mahakama za kijeshi za nchi hiyo kusikiliza kesi za raia wa kawaida nchini humo.

Hamad bin Issa Al Khalifa, Mfalme wa Bahrain, ameafiki kufanyiwa marekebisho katiba ya nchi hiyo na kuongezewa mamlaka mahakama za kijeshi za nchi hiyo baada ya kuidhinishwa na bunge la nchi hiyo.

Katiba ya Bahrain imepasishwa lengo likiwa ni kuwahukumu watu ambao wanatekeleza mashambulizi dhidi ya taasisi za kijeshi, vikosi vya nchi hiyo na vyombo vya kijeshi na kiusalama vya nchi hiyo.

Vifaru vya jeshi la Bahrain vinavyotumika kukandamiza maandamano ya wananchi 

Bunge la Bahrain tarehe 5 mwezi Machi mwaka huu liliafiki kufanyiwa marekebisho katiba ya nchi hiyo ili kuzipa mamlaka makubwa zaidi mahakama za kijeshi za nchi hiyo.

Hii ni katika hali ambayo taasisi za kutetea haki za binadamu hivi karibuni zilitoa taarifa zikisisitizia udharura wa kukomeshwa mateso wanayofanyiwa wafungwa na kutaka kupatiwa dhamana ya kulipwa fidia, kufanyika uchunguzi wa kina na wa haraka na pia kuainishwa muda kwa maripota wa Umoja wa Mataifa watakaoizuru Bahrain kwa ajili ya kuchunguza ukiukaji wa haki za binadamu wanavyofanyiwa raia wanaokamatwa.  

Wananchi wa Bahrain wamekuwa wakifanya maandamano tangu mwaka 2011 hadi hivi sasa kulalamikia siasa za kiukandamizaji za utawala wa Aal Khalifa nchini humo. Katika maandamano hayo raia wa kawaida wamekuwa wakikandamizawa vibaya na askari usalama na mamluki wao kutoka Saudia na nchi nyingine kadhaa za Kiarabu.  

Tags