Israel: Hatuhitaji baraka za Marekani kughusubu ardhi zaidi za Palestina
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i29592-israel_hatuhitaji_baraka_za_marekani_kughusubu_ardhi_zaidi_za_palestina
Waziri wa Vita wa utawala wa Kizayuni wa Israel amesema Tel Aviv haihitaji baraka wala ruhusu ya Marekani ili kuendeleza ujenzi wa vitongoji vipya vya walowezi wa Kiyahudi katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu.
(last modified 2026-01-14T08:12:18+00:00 )
May 25, 2017 09:39 UTC
  • Israel: Hatuhitaji baraka za Marekani kughusubu ardhi zaidi za Palestina

Waziri wa Vita wa utawala wa Kizayuni wa Israel amesema Tel Aviv haihitaji baraka wala ruhusu ya Marekani ili kuendeleza ujenzi wa vitongoji vipya vya walowezi wa Kiyahudi katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu.

Katika mahojiano na Idhaa ya Vita ya Israel, Avigdor Lieberman amesema Israel haijaomba wala haitawahi kuomba idhini au kibali kutoka kwa Marekani kwa ajili ya upanuzi wa vitongoji vya walowezi wake huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu.

Amesema Tel Aviv itachukua hatua kwa mujibu wa maslahi na matakwa yake bila kushauri yeyote wala kuomba idhini kwa mtu, serikali au taasisi yoyote duniani.

Matamshi ya Lieberman ni radiamali kwa hatua ya hivi karibuni ya Rais wa Marekani, Donald Trump kuutembelea utawala huo ghasibu na wakati huo huo kuitembelea Palestina inayokaliwa kwa mabavu na kukutana na kufanya mazungumzo na Mahmoud Abbas, Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina.

Trump na Mahoud Abbas

Disemba mwaka jana 2016, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipasisha maazimio yaliyoilazimisha Israel kusitisha ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi katika ardhi ya Palestina na kubomoa vitongoji vyote vilivyojengwa katika katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu.

Hata hivyo mwezi uliopita, utawala haramu wa Israel ulidharau tena maazimio hayo na kuidhinisha ujenzi wa vitongoji vipya vya walowezi wa Kiyahudi katika ardhi inayokaliwa kwa mabavu ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan huko Palestina.