Israel yatishia kumuua Katibu Mkuu wa Hizbullah
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i3691-israel_yatishia_kumuua_katibu_mkuu_wa_hizbullah
Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel ametishia kufanya mauaji ya kigaidi dhidi ya Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 24, 2016 03:35 UTC
  • Israel yatishia kumuua Katibu Mkuu wa Hizbullah

Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel ametishia kufanya mauaji ya kigaidi dhidi ya Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon.

Benjamin Netanyahu ambaye alikuwa akizungumzia matamshi yaliyotolewa na Sayyid Hassan Nasrullah kuhusu uwezo wa harakati ya Hizbullah kwa ajili ya kukabiliana na vitisho vya Israel, ametishia kuwa atamuua kiongozi huyo. Waziri Mkuu wa Israel amedai kuwa, utawala huo una azma kubwa ya kuwalenga maadui wake.

Mauaji ya kigaidi yanayofanywa na Israel dhidi ya shakhsia na watu mbalimbali si jambo geni na historia ya Palesina na Lebanon kabla na baada ya kuasisiwa utawala bandia wa Tel Aviv una mifano mingi na mauaji ya kigaidi yaliyofanywa na Wazayuni.

Mauaji ya watu wa kijiji cha Qana huko Lebanon katika muongo wa 1990 ambapo wanawake na watoto wadogo 100 waliokuwa wamekimbilia hifadhi katika makao ya Umoja wa Mataifa na kukaririwa mauaji hayo katika kijiji hicho hicho mwaka 2006 kupitia mashambulizi ya ndege za kivita za Israel katika vita vya siku 33 dhidi ya Lebanon na vilevile kuwazingira watu wa Ukanda wa Gaza na kuwamiminia mabumu na makombora ni mifano michache tu ya ugaidi wa kiserikali wa utawala haramu wa Israel.