Rais wa Palestina: Tutakata uhusiano na nchi zitakazohamishia balozi zake Quds
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i39007-rais_wa_palestina_tutakata_uhusiano_na_nchi_zitakazohamishia_balozi_zake_quds
Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina ametahadharisha kwamba, mamlaka hiyo itakata uhusiano wake na nchi yoyote ile ambayo itafuata uamuzi wa Marekani na kuuhamishia ubalozi wake huko Beitul-Muqaddas kutoka Tel-Aviv.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Jan 15, 2018 14:34 UTC
  • Rais wa Palestina: Tutakata uhusiano na nchi zitakazohamishia balozi zake Quds

Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina ametahadharisha kwamba, mamlaka hiyo itakata uhusiano wake na nchi yoyote ile ambayo itafuata uamuzi wa Marekani na kuuhamishia ubalozi wake huko Beitul-Muqaddas kutoka Tel-Aviv.

Rais Mahmoud Abbas ameashiria matokeo mabaya kwa amani ya dunia ya kutekelezwa uamuzi wa Marekani wa kuhamishia ubalozi wake Beitul-Muqaddas na kusema kwamba, kwa kuzingatia kwamba, hadi sasa watoto 2027 wa Kipalestina wameuawa shahidi kwa silaha za utawala vamizi wa Israel, Mamlaka ya Ndani ya Palestina haitakubali kuwa na uhusiano na nchi yoyote ile ambayo itaondoa ubalozi wake mjini Tel Aviv na kuuhamishia huko Beitul-Muqaddas.

Mahmoud Abbas amesisitiza kwamba, nchi yoyote ambayo itaamua kufuata uamuzi wa Marekani na kuhamishia ubalozi wake katika mji wa Beitul-Muqaddas inapaswa kutambua kwamba, Mamlaka ya Ndani ya Palestina haitakuwa na uhusiano na nchi hiyo.

Quds ni mji mkuu wa milele wa Palestina

Itakumbukwa kuwa, tarehe 6 mwezi huu wa Disemba Rais Donald Trump wa Marekani alitoa tangazo la kuitambua rasmi Beitul-Muqaddas na Kibla cha Kwanza cha Waislamu kuwa ni mji mkuu wa utawala haramu wa Israel licha ya upinzani mkubwa wa jamii ya kimataifa.

Hayo yanajiri katika hali ambayo, matokeo ya uchunguzi wa maoni kuhusiana na uamuzi wa Rais Donald Trump kuhusu Beitul-Muqaddas yanayonyesha kuwa, akthari ya raia wa nchi za Kiarabu, Kiislamu na zisizokuwa za Kiislamu wanapinga uamuzi huo wa Trump.