Mtaalamu wa kisiasa: Marekani inasababisha machafuko Afghanistan
Mtaalamu wa masuala ya kisiasa wa nchini Afghanistan amesema kuwa, nchi za eneo hili haziwezi kuamini mipango ya Marekani nchini Afghanistan, hususan juu ya madai ya viongozi wa Washington kwamba wanapambana na ugaidi na madawa ya kulevya.
Vahid Mojdeh ameashiria Kikao cha Usalama 2 kilichofanyika hivi karibuni kwa kuwashirikisha viongozi wa nchi za Afghanistan, Pakistan, Uzbekistan na Kazakhstan pamoja na makamanda wa jeshi la Marekani na Muungano wa Kijeshi wa Nchi za Magharibi (NATO) mjini Kabul, mji mkuu wa Afghanistan na kusema kuwa, kikao hicho hakikuwa na stratijia yoyote ya maana na hakitakuwa na msaada wowote kwa ajili ya usalama wa eneo hilo.
Mojdeh amengeza kuwa, licha ya juhudi za viongozi wa Marekani na NATO za kutaka kuwapa matumaini viongozi wa nchi hizo waliohudhuria kikao hicho juu ya eti kupambana kwao na wimbi la ugaidi na ongezeko la madawa ya kulevya nchini humo, viongozi hao walisisitiza kwamba hawawezi kuamini ahadi na mipango hiyo ya Washington. Kwa mujibu wa Vahid Mojdeh viongozi wa mataifa hayo walisema hayo kuwambia maafisa hao wa jeshi la Marekani na NATO kutokana na ongezeko la makundi ya kigaidi na uzalishaji wa mihadarati nchini Afghanistan.
Aidha viongozi wengi, shakhsia wa kisiasa na kidini pamoja na weledi wengi wa masuala ya kisiasa kwa mara kadhaa wamekuwa wakisisitiza kwamba, stratijia za kijeshi za Marekani katika vita vyake nchini Afghanistan zimefeli na kwamba njia pekee ya kudhamini usalama na amani ya taifa hilo ni kuondoka kwa askari wa kigeni nchini humo.