US yatumia veto kupinga azimio la kutaka kulindwa Wapalestina
Marekani imetumia kura yake ya turufu kupinga rasimu ya azimio iliyowasilishwa na Kuwait katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, ikitaka kulindwa Wapalestina katika Ukanda wa Ghaza na Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan unaokaliwa kwa mabavu.
Russia, Ufaransa na China pamoja na nchi nyingine saba wanachama wa Baraza la Usalama zimepiga kura ya ndio kuunga mkono rasimu hiyo, huku nchi nyingine nne ikiwemo Uingereza zikijizuia kupiga kura.
Riyadh Mansour, Balozi wa Palestina katika umoja huo sanjari na kulaani kitendo hicho cha uhasama cha Marekani, ameitaka jamii ya kimatiafa itafute mbinu mpya ya kukabiliana na namna Washington inavyotumia vibaya kura yake ya turufu au veto katika Baraza la Usalama la UN kwa ajili ya kuutetea utawala wa Kizayauni unaotenda jinai dhidi ya Wapalestina.
Tokea Machi 30 hadi sasa, utawala haramu wa Israel umewaua shahidi Wapalestina zaidi ya 120 mbali na kujeruhi wengine 13,300, kwa kushiriki katika maandamano ya kutetea haki ya kurejea katika ardhi zao za jadi.
Mwishoni mwa mwaka jana pia, na licha ya wanachama 14 wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuupigia kura ya ndio muswada uliopendekezwa na Misri kuhusu mji mtakatifu wa Baytul Muqaddas, lakini Marekani iliukwamisha muswada huo kwa kura yake ya veto.
Muswada wa azimio hilo ulikuwa umesema: Uamuzi au hatua yoyote yenye nia ya kubadilisha utambulisho, hali au muundo wa kijamii wa mji mtakatifu wa Quds, haina athari za kisheria na inabidi ifutwe kwa mujibu wa maazimio ya Umoja wa Mataifa.