Russia: Wakimbizi 270,000 wa Syria wamerejea nyumbani
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i49556-russia_wakimbizi_270_000_wa_syria_wamerejea_nyumbani
Jeshi la Russia limetangaza habari ya kurejea nyumbani wakimbizi zaidi ya laki mbili na 70 elfu wa Syria ndani ya miezi michache iliyopita.
(last modified 2025-11-07T02:31:33+00:00 )
Nov 16, 2018 14:53 UTC
  • Wakimbizi wa Syria wakirejea nchini kwao.
    Wakimbizi wa Syria wakirejea nchini kwao.

Jeshi la Russia limetangaza habari ya kurejea nyumbani wakimbizi zaidi ya laki mbili na 70 elfu wa Syria ndani ya miezi michache iliyopita.

Kanali Jenerali Mikhail Mizintsev wa Wizara ya Ulinzi ya Russia amewaambia waandishi wa habari leo Ijumaa kuwa, wiki iliyopita pekee, wakimbizi 6,000 walirejea nchini Syria na kwamba makundi mengi ya wakimbizi hao yako njiani kurejea nyumbani. 

Hivi karibuni pia, mamia ya wakimbizi wa Syria walivuka kivuko cha mpakani cha Abu Dhuhur na kurejea katika maeneo yao baada ya jeshi la nchi hiyo kuwafurusha magaidi katika maeneo ya kaskazini mwa nchi hiyo.

Hivi sasa juhudi zinaendelea za kuwarejesha nyumbani wakimbizi hao katika maeneo yaliyokombolewa na serikali kutoka mikononi mwa magenge hatari ya kigaidi na ya wakufurishaji.

Ushirikiano wa Russia, Iran na Syria dhidi ya magenge ya kigaidi

Takwimu za Umoja wa Mataifa zinaonesha kuwa, karibu raia milioni 7 wa Syria wamekuwa wakimbizi kutokana na mgogoro wa zaidi ya miaka saba sasa wa ndani ya nchi yao.

Mgogoro nchini Syria uliibuka mwaka 2011 baada ya makundi ya kigaidi yanayosaidiwa na kuungwa mkono na Saudia, Marekani, Israel na washirika wao kuanzisha mashambulizi makubwa kwa lengo la eti kuleta mlingano wa nguvu na mabadiliko katika eneo la Mashariki ya Kati kwa maslahi ya utawala haramu wa Israel. Hata hivyo njama hizo zimefeli kwa mapambano na kusimama imara viongozi na raia wa Syria.