Wafaransa wawafundisha magaidi namna ya kutumia silaha za kemikali nchini Syria
(last modified Thu, 22 Nov 2018 14:45:25 GMT )
Nov 22, 2018 14:45 UTC
  • Wafaransa wawafundisha magaidi namna ya kutumia silaha za kemikali nchini Syria

Shirika la habari la Sputnik limenukuu duru moja ya kuaminika ikisema kuwa wataalamu wa kemikali wa Ufaransa wanawafundisha magaidi mbinu za kutumia silaha za kemikali nchini Syria.

Shirika hilo la Sputnik la nchini Russia limeinukuu duru moja iliyoko karibu na makamanda wa kijeshi wa Syria akisema leo Alkhamisi kwamba, wataalamu wa Ufaransa wanatoa mafunzo na kuwasaidia magaidi mbinu za kutumia silaha za kemikali na jinsi ya kubeba vichwa vya silaha hizo hatari.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, watu wanaojulikana kwa jina maarufu la wavaa kofia nyeupe wamewapelekea magaidi walioko mjini Idlib mabomu matano ya gesi za sumu.

Mamluki wa madola ya Magharibi waliojipenyeza nchini Syria kuwasaidia magaidi kwa jina la misaada na kulinda haki za binadamu ni maarufu kwa jina la wavaa kofia nyeupe

 

Ripoti hiyo imeongeza kuwa, mabomu hayo matano wamekabidhiwa wataalamu wa kemikali wa Ufaransa walioingia mjini Idlib hivi karibuni ili wayatumie kutengeneza makombora yenye uwezo wa kubeba vichwa vya kemikali na gesi za sumu.

Ikumbukwe kuwa Ufaransa ni moja ya waungaji mkono wakuu wa magenge ya kigaidi tangu ilipovamiwa nchi ya Kiarabu ya Syria mwaka 2011.

Duru huru zimeshatoa ripoti nyingi zinazoonesha jinsi magaidi wanaoungwa mkono na madola ya kibeberu ya Magharibi ikiwemo Ufaransa wanavyotumia silaha za kemikali dhidi ya wananchi wa kawaida nchini Syria.