Makundi ya Muqawama Palestina: Marekani, Israel zimepata pigo kubwa UN
(last modified Fri, 07 Dec 2018 14:37:44 GMT )
Dec 07, 2018 14:37 UTC
  • Makundi ya Muqawama Palestina: Marekani, Israel zimepata pigo kubwa UN

Makundi ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina ya Hamas na Jihadu Islami yamesema kupigwa mweleka katika Baraza la Kuu la Umoja wa Mataifa muswada wa kuilaani Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) na kuitaja kama kundi la kigaidi ni pigo kubwa kwa Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Muswada huo ulizitaka nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kuilaani harakati ya Hamas na mashambulizi yake ya makombora dhidi ya maeneo ya jeshi la Israel na vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu.

Fawzi Barhoum, Msemaji wa Hamas sambamba na kuzishukuru na kuzipongeza nchi zilizoupigia kura ya la muswada huo, amesema hatua hiyo kwa mara nyingine tena umeweka wazi kuwa mapambano ya ukombozi ya watu wa Palestina ni halali.

Naye Dawoud Shahab, Msemaji wa Jihadu Islami amesema kushindwa muswada huo katika Baraza Kuu la UN ni pigo jingine kubwa kwa tabia ya kueneza urongo na propaganda ya serikali ya Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel.

 

Baraza Kuu la UN

Amesema nchi zilizopiga kura ya ndio kuunga mkono muswada huo wa Marekani zimepata fedheha kubwa; na unafiki, woga na tabia yao ya kutopenda ukweli na haki imeanikwa wazi.

Muswada huo uliopigiwa kura alasiri ya jana katika Baraza Kuu la UN ulipata kura 86 za ndio, 58 za kupinga huku nchi nyingine 33 zikijizuia kuupigia kura. Muswada huo wa Marekani dhidi ya Hamas ulipaswa kupata kura zisizopungua 99 kwa ajili ya kupasishwa na kuilaani Hamas na kuitaka kuwa ni kundi la kigaidi.

 

Tags