Lebanon kuishtaki Israel Baraza la Usalama la UN
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i50450-lebanon_kuishtaki_israel_baraza_la_usalama_la_un
Waziri wa Mambo ya Nje wa Lebanon amemtaka mwakilishi wa kudumu wa nchi hiyo katika Umoja wa Mataifa kuwasilisha mashtaka dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel katika Baraza la Usalama la umoja huo baada ya utawala huo kutumia anga ya Lebanon katika mashambulizi yake nchini Syria.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 27, 2018 03:24 UTC
  • Gebran Bassil
    Gebran Bassil

Waziri wa Mambo ya Nje wa Lebanon amemtaka mwakilishi wa kudumu wa nchi hiyo katika Umoja wa Mataifa kuwasilisha mashtaka dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel katika Baraza la Usalama la umoja huo baada ya utawala huo kutumia anga ya Lebanon katika mashambulizi yake nchini Syria.

Katika taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Lebanon Gebran Bassil amelaani mashambulizi ya ndege za kivita za Israel dhidi ya Syria na kusisitiza haki ya Lebanon ya kulinda ardhi na mamlaka yake.

Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Lebanon imesema kuwa mashambulizi ya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Syria ni hatari na tishio kwa amani na usalama wa Mashariki ya Kati na imeitaka jamii ya kimataifa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kulaani mashambulizi hayo na vilevile kitendo cha Israel cha kutumia anga ya Lebanon kwa ajili ya kuishambulia nchi rafiki, suala ambalo linakinzana na azimio nambari 1701 la Baraza la Usalama. 

Jana usiku ndege za kivita za Israel zilikiuka anga ya Lebanon na kufyatua makombora 16 kuelekea mji mkuu wa Syria, Damascus. Hata hivyo Jeshi la Anga la Syria limefanikiwa kutungua makombora ya ndege hizo kabla ya kulenga shabaha. 

Israel ambayo ilikuwa ikiwaunga mkono na kuwasaidia magaidi wa makundi mbalimbali hususan Daesh huko Syria sasa inatapatapa baada ya makundi hapo kupata kipigo cha mbwa na magenge yao kusambaratika.