'Utawala wa Kizayuni wa Israel ni adui namba moja wa Pakistan'
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i52038-'utawala_wa_kizayuni_wa_israel_ni_adui_namba_moja_wa_pakistan'
Waziri wa Nchi wa Pakistan anayehusika na masuala ya Bunge amesema, utawala haramu wa Kizayuni wa Israel ni adui namba moja wa nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 09, 2019 00:52 UTC
  • 'Utawala wa Kizayuni wa Israel ni adui namba moja wa Pakistan'

Waziri wa Nchi wa Pakistan anayehusika na masuala ya Bunge amesema, utawala haramu wa Kizayuni wa Israel ni adui namba moja wa nchi hiyo.

Ali Muhammad Khan ametoa sisitizo hilo katika hotuba aliyotoa mbele ya Baraza la Seneti la Pakistan na kubainisha kuwa, utawala wa Kizayuni ni adui namba moja wa Wapakistan na kwamba Islamabad katu haitautambua rasmi utawala huo.

Waziri wa Nchi wa Pakistan an anayehusika na masuala ya Bunge ameongeza kuwa, serikali ya Waziri Mkuu Imran Khan haifikirii abadani kujadili suala la kuutambua rasmi utawala wa Kizayuni wa Israel na wala haitasalimu amri mbele ya watu wanaozungumzia kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala huo.

Ali Muhammad Khan amesisitiza pia kwamba wananchi wote wa Pakistan wameungana na wako kitu kimoja katika msimamo wa kupinga kuanzisha uhusiano na utawala wa Kizayuni.

Serikali ya Islamabad imetangaza msimamo huo wakati nchi kadhaa za Kiarabu zikiongozwa na Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) zinapigana vikumbo, kwa kila moja kutaka iwe ya mbele katika kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Kizayuni unaoikalia kwa mabavu Palestina na kibla cha kwanza cha Waislamu.../