Hizbullah: Utawala haramu wa Israel ndio chimbuko kuu la ugaidi duniani
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i52964-hizbullah_utawala_haramu_wa_israel_ndio_chimbuko_kuu_la_ugaidi_duniani
Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Kiislamu ya Hizbullah nchini lebanon, Sheikh Naim Qassem amesema kuwa, utawala haramu wa Kizayuni wa Israel ndio chanzo kikuu cha ugaidi na uharibifu katika eneo la Asia Magharibi na duniani kwa ujumla.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 19, 2019 23:54 UTC
  • Hizbullah: Utawala haramu wa Israel ndio chimbuko kuu la ugaidi duniani

Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Kiislamu ya Hizbullah nchini lebanon, Sheikh Naim Qassem amesema kuwa, utawala haramu wa Kizayuni wa Israel ndio chanzo kikuu cha ugaidi na uharibifu katika eneo la Asia Magharibi na duniani kwa ujumla.

Sheikh Naim Qassem ameongeza kwamba kuanzisha vita, uvamizi na kutenda jinai mbalimbali zisizokubalika, ndio kazi na sifa halisi ya utawala huo katili.

Amesisitiza kwamba, muqawama utaendelea kusimama imara kukabiliana na vitisho vya utawala huo na Marekani kama ambavyo pia utasimama dhidi ya matatizo na vikwazo ilivyowekewa.

Akibainisha kwamba, lau kama si Harakati ya Hizbullah hii leo Israel ingekuwa haijaondoka ndani ya maeneo ya Lebanon, genge la Daesh (ISIS) lingekuwa halijashindwa na nchi za eneo zingekuwa hatarini amesema kuwa, chaguo la muqawama, ni chaguo la ushindi na kujitegemea na kwamba chaguo hilo kamwe halitalegezwa kamba.

Sheikh Naim Qassem, Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah

Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ameashiria uwepo wa matatizo ya kiuchumi na kifedha nchini Lebanon na kusema kuwa pande zote zinatakiwa kushirikiana kwa ajili ya kutatua tatizo hilo, kwani bila ya mshikamano na kusaidiana, matatizo hayatopata ufumbuzi. Hatua ovu za utawala haramu wa Kizayuni katika eneo la Asia Magharibi zinazofanyika mbele ya kimya cha kimataifa ukiwemo Umoja wa Mataifa, zimeufanya utawala huo khabithi kupata kiburi cha kuendeleza jinai zake za kila leo.