Dec 05, 2019 01:21 UTC
  • Uwepo wa askari wa Kimarekani Afghanistan, chanzo cha ukosefu wa ajira

Uchunguzi uliofanywa hivi karibuni nchini Afghanistan umeonyesha kwamba, uwepo wa askari vamizi wa Kimarekani ndio sababu ya kuongezeka kiwango cha ukosefu wa ajira kwa raia wa nchi hiyo.

Matokeo ya uchunguzi huo uliofanywa na taasisi ya 'Bunyad Asia' katika majimbo 34 ya Afghanistan na kutolewa siku ya Jumanne iliyopita, yanaonyesha kwamba asilimia 72 ya vijana wa taifa hilo wanakabiliwa na tatizo kuu la ukosefu wa ajira. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, zaidi ya raia elfu 17, 800 ambao walishirikishwa katika uchunguzi huo, walisema kwamba kiwango cha nafasi za kazi ikilinganishwa na mwaka mmoja uliopita, kimepungua kwa asilimia 50. Kabla ya hapo pia kiwango cha takwimu za ukosefu wa ajira nchini Afghanistan kilitangazwa kuwa ni asilimia 40.

Askari wa kigeni nchini Afghanistan sababu ya kukithiri ugaidi na ghasia nchini humo

Aidha uchunguzi huo unaonyesha kwamba kuendelea kwa vita na mashambulizi ya kigaidi ni mambo yanayochangia ongezeko la kiwango cha ukosefu wa ajira katika nchi hiyo. Ongezeko la machafuko na shughuli za makundi ya kigaidi nchini humo linajiri katika hali amabyo Marekani na washirika wake waliivamia Afghanistan mwaka 2001 kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi na kurejesha usalama nchini humo. Hata hivyo viongozi wa Kabul wamekuwa wakikariri mara kwa mara kwamba uwepo wa askari wa Marekani nchini humo si tu kwamba umesababisha kuongezeka machafuko, bali umepelekea pia kuongezeka ugaidi na uzalishaji wa madawa ya kulevya.  

Tags