Mar 08, 2020 12:22 UTC
  • Mwanamfalme wa nne atiwa mbaroni nchini Saudi Arabia

Duru za habari za karibu na utawala wa kifalme wa Saudia zimeripoti habari ya kutiwa mbaroni mwanamfalme wa nne kwa amri ya Mrithi wa Kiti cha Ufalme wa nchi hiyo.

Kwa mujibu wa habari hiyo, Nayef Bin Ahmed, ni mwanamfalme wa nne wa Saudia ambaye aliwahi kuongoza Intelijensia ya jeshi la Saudia na ametiwa mbaroni kwa amri ya Mohammad Bin Salman, Mrithi wa Kiti cha Ufalme wa nchi hiyo. Ijumaa iliyopita pia Ahmed bin Abdulaziz Al Saud, ndugu yake Mfalme Salman bin Abdulaziz, Muhammad bin Nayef, Mrithi wa Kiti cha Ufalme wa zamani na Nawaf bin Nayef, ndugu yake mdogo, walitiwa mbaroni kwa tuhuma za uhaini kupitia amri ya Muhammad Bin Salman. Gazeti la Uingereza la Middle East Eye limezinukuu duru za habari juu ya uwezekano wa kunyongwa au kuhukumiwa vifungo vya maisha wanawafalme hao waliotiwa mbaroni.

Mohammad Bin Salman, Mrithi wa Kiti cha Ufalme wa Saudia

Kwa mujibu wa watu wa karibu na ufalme wa Saudia, kamatakamata ya hivi karibuni dhidi ya wanawafalme inatokana na wasi wasi mkubwa wa Mohammad Bin Salman, juu ya njama za shakhsia wa ukoo huo kumpindua. Aidha wameongeza kuwa wasi wasi huo unaonyesha kwamba mrithi huyo wa kiti cha ufalme anafanya kila analoweza kufyeka kila aina ya upinzani kati ya wanaukoo huo.

Tags