Jul 19, 2020 02:49 UTC
  • Yedioth Ahronoth: Benjamin Netanyahu ni kirusi hatari mno

Gazeti la Kizayuni la Yedioth Ahronoth limechapisha makala inayomkosoa vikali Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na kueleza kuwa, mwanasiasa huyo ni kirusi hatari mno.

Makala hiyo mbali na kumpa Netanyahu jina la "kirusi hatari" imemkosoa Waziri Mkuu huyo wa utawala haramu wa israel kutokana na utendaji dhaifu mno wa baraza lake la mawaziri katika kukabiliana na virusi vya corona.

Gazeti hilo linaeleza kwamba, baraza la mawaziri la Israel limeshindwa kabisa kukabiliana na ueneaji wa virusi vya corona ambapo wahanga wake wamekuwa wakiongezeka kila leo huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu (Israel).

Maandamano dhidi ya Benjamin Netanyahu huko Tel Aviv

Katika seghemu nyingine ya makala hiyo, gazeti hilo la Yedioth Ahronoth limeashiria mgogoro mkubwa wa kiuchumi unaowakabili Wazayuni na kubainisha kwamba, anachokifuatilia Netanyahu kwa sasa ni kulipa fedha nyingi kwa ajili ya kujitetea katika faili la ufisadi linalomkabili.

Ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu (Israel) kwa mara ya kadhaa zimeshuhudia maandamano mtawalia ya wananchi katika kipindi cha miezi miwili ya hivi karibuni dhidi ya Baraza la Mawaziri la Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu.

Wiki iliyopita wakazi wa Palestina inayokaliwa kwa mabavu (Israel) walifanya maandamano makubwa na kisha kukusanyika mbele ya makao ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu na kutoa wito wa kujizulu kiongozi huyo wakisema kuwa, ameshindwa kuyapatia ufumbuzi matatizo yanayowakabili.

Tags