Kiongozi wa Ansarullah: Mapinduzi ya Septemba 21 ya wananchi wa Yemen yalikuwa mwanzo wa kuondokana na giza la huko nyuma
-
Sayyid Abdulmalik al Houthi
Kiongozi wa harakati ya Ansarullah ya Yemen amesema kuwa mapinduzi ya tarehe 21 Septemba nchini humo yalikuwa mwanzo wa kupatikana njia ya kujiondoa katika giza la huko nyuma na hatua ya kujenga mustakbali kwa mujibu wa thamani na misingi ya watu wa Yemen.
Sayyid Abdulmalik al Houthi ameongeza kuwa lengo kuu zaidi la mapindzi hayo ni kujikomboa na kuwa huru nchi ya Yemen. Kiongozi huyo wa harakati ya Ansarullah aliyasema hayo jana katika hotuba iliyotolewa kwa mnasaba wa madhimisho ya mapinduzi ya Septemba 21 nchini humo.
Abdulmalik al Houthi ameongeza kuwa, mfumo wa kisiasa uliopita haukuwa na ufahamu kuhusu uwezo wa wananchi wa Yemen na uliamini kwamba wananchi hawawezi kusimama kidete mbele ya uingiliaji wa Marekani na kulinda kujitawala na uhuru wao.
Al Houthi ameashiria pia matatizo yanayowakabili watu wa Yemen na kusema: Ugumu wa maisha unaowasibu Wayemeni ni matokeo ya vita vya pande dhidi ya taifa hilo, kuzingirwa nchi na kuzuia kuingizwa mafuta na mapatano yanayotokana na bidhaa hiyo.
Wananchi wa Yemen tarehe 21 Septemba mwaka 2014 walifanya maandamano ya nchi nzima wakilalamikia utendaji dhaifu wa serikali ya muda ya Abdu Rabbu Mansour Hadi katika kusimamia masuala ya nchi; na harakati ya Ansarullah ilichukua uongozu baada ya kuingia katika mji mkuu wa nchi hiyo, Sana'a.

Sayyid Abdulmalik al Houthi ameashiria pia mapatano yaliyofikiwa kati ya Imarati na Bahrain na utawala wa Kizayuni wa Israel na kusema: Ikiwa Saudi Arabia ilikuwa ng'ombe ya kukamwa maziwa ya Marekani basi Imarati nayo ni mbuzi wa maziwa wa nchi hiyo.