Jun 24, 2021 03:37 UTC
  • Al Wifaq: Utawala wa Aal Khalifa ni wa kizamani

Jumuiya ya Kiislamu ya Bahrain ya al Wifaq imesisitiza juu ya ulazima wa kutekelezwa marekebisho makubwa na mapana nchini humo na kueleza kuwa utendaji uliopitwa na wakati wa utawala wa Aal Khalifa hauwiani na mazingira ya sasa.

Katika taarifa yake ya jana, Jumuiya ya al Wifaq imeweka wazi vipengee saba vya marekebisho na kueleza kuwa utawala wa Aal Khalifa unapasa kutekeleza marekebisho hayo haraka iwezekanavyo. 

Taarifa ya Al Wifaq imeeleza kuwa, utawala wa Aal Khalifa inatumia mbinu zote za ukandamizaji kuwanyamazisha wananchi wanamapinduzi wa Bahrain. Imesema uhuru wa kusema haupo tena huko Bahrain. Watu wote wanaoukosoa utawala huo ulioko madarakani wanaadhibiwa. Taarifa ya Jumuiya ya Kiislamu ya al Wifaq imeendelea kueleza kuwa: Utawala wa Aal Khalifa unastafidi na mbinu za kizamani kuendesha nchi na kwamba kuna ulazima wa kubuniwa mfumo wa kisheria wa kiadilifu huko Bahrain na mafisadi waondolewe katika taasisi za usalama na kijeshi. 

Sehemu nyingine ya taarifa ya Jumuiya ya al Wifaq imesema: 'Utawala wa Aal Khalifa hauna uwezo wa kuchukua maamuzi katika nyuga za kisiasa, kiusalama na kidiplomasia. Utawala huo unachukua maamuzi kwa maslahi ya wengine tu. Kuna ulazima wa kupewa kipaumbele maslahi ya taifa la Bahrain', inamalizia taarifa hiyo. 

Wananchi wa Bahrain wamekuwa wakifanya maandamano dhidi ya utawala wa Aal Khalifa kuanzaia mwaka 2011 hadi sasa wakitaka kufanyika marekebisho makubwa nchini humo. 

Maandamano ya wananchi wa Bahrain dhidi ya utawala ulioko madarakani

 

Tags