"Muqawama wa Kiislamu utajibu hujuma zote za Israel dhidi ya Lebanon"
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i73466-muqawama_wa_kiislamu_utajibu_hujuma_zote_za_israel_dhidi_ya_lebanon
Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amesema utawala wa Kizayuni wa Israel unapaswa kufahamu kuwa, muqawama wa Kiislamu utatoa majibu kwa mashambulizi yote ya Tel Aviv dhidi ya Lebanon.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 13, 2021 08:33 UTC

Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amesema utawala wa Kizayuni wa Israel unapaswa kufahamu kuwa, muqawama wa Kiislamu utatoa majibu kwa mashambulizi yote ya Tel Aviv dhidi ya Lebanon.

Sheikh Naim Qassim amesema hayo katika hotuba yake aliyoitoa kwa mnasaba wa maombolezo ya Muharram katika eneo la Ouzai na kuongeza kuwa, muqawama wa Kiislamu umeleta mlingano madhubuti wa kuzima chokochoko za adui Mzayuni.

Sheikh Qassim ameashiria hatua ya Israel kushambulia kijeshi eneo la kusini mwa Lebanon hivi karibuni, likiwa shambulio la kwanza la aina hiyo tangu mwaka 2006 na kusisitiza kuwa, jibu la Hizbullah kwa uchokozi huo mpya wa Wazayuni lilionesha wazi kuwa mrengo huo wa muqawama una uungaji mkono madhubuti wa wananchi wa Lebanon.

Utawala huo haramu bila kutoa ushahidi wowote ulidai kuwa, shambulio lake la anga dhidi ya eneo la kusini mwa Lebanon ni jibu eti kwa mashambulio ya makombora yaliyotokea kusini mwa hiyo ya Kiarabu.

Wanamuqawama wa Hizbullah

Sheikh Naim Qassim amesema picha za Hizbullah wakisherehekea ushindi baada ya kutoa kipigo kikali mkabala wa uchokozi wa Israel katika mji wa Khiyam wakiwa pamoja na wakazi wa kijiji cha Druze zimewafedhehesha Wazayuni wanaojaribu kuihadaa dunia kuwa harakati hiyo haiungwi mkono na wananchi. 

Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amesema mrengo huo wa muqawama unajivunia mkakati wa aina yake wa kuwa na kambi ya mapambano inayojumuisha askari na raia wa kawaida.