May 20, 2016 07:03 UTC
  • Mamia ya magaidi waangamizana nchini Syria

Mamia ya magaidi wameangamizana katika viunga vya Damascus, mjini mkuu wa Syria baada ya kutokea mapigano makali baina yao.

Shirika la habari la al Ahd la nchini Lebanon limetangaza habari hiyo na kuongeza kuwa, mapigano makali yanaendelea baina ya genge ya kigaidi katika eneo la Ghouta Mashariki, nje ya mji wa Damascus, na hadi jana yalikuwa yamesababisha magaidi 800 kuuawa.

Mizozo baina ya magenge ya kigaidi nchini Syria inatokana na kuwania maeneo zaidi ya udhibiti wa makundi hayo ya kitakfiri.

Kwa upande wake, jeshi la Syria limeendelea na operesheni za kupambana na magenge ya kigaidi katika vitongoji vya Deir al Asafir na Zebdeen huko Ghouta Mashariki na kufanikiwa kuvidhibiti kikamilifu vitongoji hivyo viwili baada ya kuwafurusha magaidi.

Vikosi vya jeshi la Syria jana vilifanikiwa pia kuingia katika kitongoji cha Bazina, huko Ghouta Mashariki nje ya mji wa Damascus na kutegua mabomu yaliyokuwa yametengwa na magenge ya kigaidi.

Mgogoro wa Syria ulizushwa mwaka 2011 baada ya magenge mengi ya kigaidi yanayoungwa mkono na Markeani na waitifaki wake kuanzisha wimbi kubwa la mashambulizi kwa lengo la kuipindua serikali ya Rais Bashar al Assad wa nchi hiyo, licha ya serikali hiyo kuchaguliwa kihalali kwa kura za wananchi.

Tags